Makongoro ameyasema hayo akiwa kampene za uchaguzi mkoani Njombe wakati akimnadi mgombea wa Uraisi kupitia chama cha Mapinduzi CCM na mgombea wa Ubunge wa jimbo la Njombe Kusini Juzi.
Alisema sema kuwa mgombea urais kupitia Chadema na kuungwa mkono na Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa Edward Lowassa anaumwa na waziri mkuu wa zamani Fredrick Sumaye anasubili kuwa Rais Kilaka baada ya mgombea Urais Kupata matatizo.
Alisema kuwa kuna mwaka uchaguzi ulisubilishwa kwa sababu mgombea alifariki na kuwekwa mgombea Mwingine wa kilaka kwaajili ya kuziba pengo.
"Kakayangu Sumaye anasubuli Lowassa afariki ndipo yeye awe kilaka kugombea nafasi ya urais, hatutaki raisi kilaka tunataka rais mzima Mchagueni Maguruli," alisema.
Makongoro alisema kuwa watanzania wamchague Dr. John Magufuli kwaajili ya maendeleo na kuwa magufuri ukilinganisha na Mgombea wa Ukawa Lowassa kiafya Magufuri yupo ngangali.
Aliongeza kuwa Magufuli baada ya kuingia Ikulu ata hakikisha kuwa anarekebisa mikataba ya madini na kuwa kwa sasa migodi ya Nyamongo wawekezaji wanachukua asilimia 70 na Tanzania asilimia 30 atabadilisha na watanzania kuanza kunufaika.
Alisema kuwa katika nchi zenye utajiri hapa ulimwenguni wa banini Tanzania nayo imo na kuwa nchi hii ni tajiri sio watu wake.
Aliongeza kuwa Ukawa wanasema wao matajiri utajiri ni wa nchi sio wa mtu mmoja mmoja na usema kuwa baada ya kuanza uchimbaji wa madini serikali itaaza kuchukua pesa zitokanazo na madini na kufanya maendeleo na watanzania kuanza kunufaika.