Showing posts with label Ukawa. Show all posts
Showing posts with label Ukawa. Show all posts
BARAZA LA MAWAZIRI VIVURI HILI HAPA

BARAZA LA MAWAZIRI VIVURI HILI HAPA

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani  Freeman Mbowe.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Freeman Mbowe.
Hatimaye, Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ametangaza baraza lake la mawaziri kivuli leo bungeni mjini Dodoma.
Aidha, Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema ametaja baraza lake ambalo litakuwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Rais Magufuli kutimiza kile alichoahidi kwa Watanzania.
Baraza hilo la Mawaziri litakuwa na kazi kubwa ya kuendana na kauli Mbiu ya Chama cha Mapinduzi ya Hapa Kazi tu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Baraza zima la Kambi rasmi ya Upinzani   ni kama ifuatavyo;
1.Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel
2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul
3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla
4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Magdalena Sakaaya
Naibu Waziri – Emmaculate Swari
5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri-Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha
6.Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde
7.Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche
8.Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri – Tundu Lissu
Naibu Waziri Abdalla Mtolela
9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal
10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara
11.Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla
12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso
13.Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso
14.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe
15.Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph
16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul
17.Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja
18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Hamidu Hassan
Naibu Waziri– Peter Lijualikali


UKAWA Wasimulia Kilichowafanya Walete Vurugu Na Kumzomea Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein


UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema mipango yao ya kutomruhusu Rais Dk. John Magufuli kulihutubia Bunge akiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, imefanikiwa.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Freeman Mbowe, alisema jana kuwa walimua kuzuia Rais Magufuli asihutubie Bunge kwa vile Dk. Shein, muda wake wa kuwa rais ulikwisha tangu Novemba 2 mwaka huu kwa hiyo hakustahili kuhudhuria Bunge hilo.

Alisema kuwa waliamua kufanya vile wakiamini kuwa ilikuwa sehemu muafaka ya kufikisha kilio chao kutokana na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano ule, wakitokea katika nchi za jumuiya ya kimataifa.

“Tulishangaa kumuona Dk. Shein, Pandu Amiri Kificho na Makamu wa Pili wa Rais wakiwa ndani ya Bunge wakati kikatiba hawana uhalali,” alisema Mbowe.

Alisema, baada ya kitendo kile hivi sasa umoja wa vyama hivyo, unatarajia kukutana ili kupeana mikakati ya kuendeleza mapambano ya ndani na nje ya nchi ya kudai haki.

“Uchaguzi wa Zanzibar hauwezi kutenganishwa kikatiba au kisiasa na uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya muungano,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema Ukawa hawako tayari kuinajisi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu viongozi wasio halali kuingia bungeni.

Aidha, Mbowe alisema walitaka shughuli ya ufunguzi rasmi wa Bunge isitishwe kwa sasa na kuahirishwa hadi hapo Rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, atakapotangazwa rasmi na kuapishwa.

Naye Mwenyekiti Mwenza, James Mbatia, alisema haijawahi kutokea katika historia ya Bunge tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kwa vyombo vya dola kuingia ndani ya bunge na kuwatoa wabunge kwa nguvu.


“Wakati sisi tunatafuta majadiliano mezani ilikumaliza mgogoro huu wenzetu Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameamua kutumia majeshi kukandamiza demokrasia,” alisema Mbatia.


Mbatia alisema kuwa hawatakaa kimya bali wataendelea kupigania matakwa ya wananchi hususan kwa upande wa Zanzibara.

“Kuna mambo mengi yanafanywa hovyo na CCM na wapinzani wamekuwa wakivumilia kwa sababu ya kumpenda mama Tanzania lakini hivi sasa wasijaribu kuharibu amani, utulivu na mshikamano uliopo,” alisema.

Mbatia, alisema kwa kawaida mtu anapodhulumiwa haki yake kila mara matokeo yake anachoka kwa hiyo kuna siku ataifuta haki yake hata kwa kusababisha kumwaga damu.

Naye Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa ) wamesikitishwa na kitendo cha serikali ya CCM kuonesha wazi jinsi walivyobaka na kuikanyaga demokrasia nchini.

Alitoa kauli hiyo aipokuwa akizungumza na mwandishi wetu muda mfupi baada ya kutoka bungeni baada ya kufukuzwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya wabunge wa umoja huo kupinga kitendo cha kuruhusiwa kwa Rais wa Zanzibar kuwa sehemu ya Bunge.

Lissu alisema imeonesha wazi kuwa serikali ya CCM ilivyo kuwa ikitumia mabavu ya kuvunja sheria waziwazi sambamba na kuvunja kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari kwa afya ya nchi.

Akizungumzia kutoka kwao nje ya ukumbi wa Bunge alisema serikali ya CCM kwa kutumia kiti cha Spika walionekana kupanga mbinu chafu za kuwazima wabunge wa Ukawa ili wasiweze kufikisha hoja zao mbele za wananchi kupitia bunge hilo.

“Unaweza kuona kwamba serikali ya CCM inavyoweza kuvitumia vibaya vyombo vya dola, kwa utaratibu jinsi ulivyo ili kuruhusu watu waingie katika ukumbi wa bunge ni lazima kutengua kanuni ili watu waeze kuingia lakini kutokana na uovyo na ujinga mkubwa wa serikali ya CCM, ambayo haizingatii sheria na katiba imeweza kuleta askari wengi pamoja na majeshi kwa ajili ya kukabiliana na upinzani.

“Jambo kubwa na baya zaidi na la ajabu ni pale ambapo askali waliovaa magwanda ya polisi na jeshi wakiwa na silaha za moto walivyoweza kuingia katika ukumbi wa bunge kwa misingi ya kutaka kukabiliana na wabunge wa upinzani.

“Jambo hapa ni kwamba hata wao wanajua kuwa Dk. Shein siyo rais halali wa Zanziba lakini kwa ubishi wao wanalazimisha kufanya hivyo na kutokana na hali hiyo ndiyo maana serikali imekuwa ikitumia vyombo vya dola kwa ajili ya kuthibiti wabunge wa Upinzania ambao wametumwa na Umma wasitoe mawazo yao,” amesema Lissu.

Mbali na hilo alisema pamoja na kuwa walizuiliwa kuendelea na bunge, kwa ajili ya kuwasilisha hoja zao kwa watanzania lakini watatumia mbinu nyingi za kufikisha ujumbe kwa jamii kwani kwa sasa kuna kila mikakati ya kuhakikisha wanataka kuuzima upinzani.

Akizungumzia kuhusu kanuni za bunge kwa sasa alisema kama ilivyo katiba ya sasa ilivyo na makosa kibao ndivyo na kanuni za bunge zinavyotakiwa kurekebishwa kwani kuna makosa mengi zaidi.

Kwa upande wao wabunge wa Zanzibar walisema ni dhambi kubwa kwa Dk. Ali Mohamed Shein kuenedelea kung’ang’ania kukaa madarakani wakati muda wake umeisha jambo ambalo linaonesha wazi kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka na dola yake.

“Inasikisha zaidi kuona jinsi Rais wa Zanzibar alivyokuwa siyo muungwana anajua kabisa kwamba hakushinda uchaguzi, lakini ikumbukwe wakati wa kuvunja baraza la wawakirishi wabunge wa CCM walimkataa Maalim Seif Shariff Hamad kama makamu wa kwanza wa rais asiingie katika bunge.


“Lakini kwa uungwana wa kiongozi huyo aliondoka wala hakuhudhuria kikao hicho lakini jambo la kushangaza huyu Dk. Shein amekomaa sasa inafikia hatua anazomewa bila kuwa na aibu sasa huo ni uongozi gani na anamuongoza nani,” amesema.


“Tunamuuliza Rais Magufuli, ni nani akapeleka vifaru na kuongeza askari wengi katika nchi za Zanzibar na ni kwa sababu gani.

“Kwa sasa hali ya Zanzibar si shwali kwani kila jambo sasa limelala kwani hata watalii hawaji kama ilivyokuwa mwanzo, mbali na hilo kuna hali ya sitofahamu ni kwani nguvu nyingi ya vyombo vya dola inaelekezwa Zanzibar,” alisema mmoja wa wabunge wa Zanzibar.
Ukawa wapitisha majina mawili kusaka uspika na Unaibu

Ukawa wapitisha majina mawili kusaka uspika na Unaibu


Baada ya mchakato wa ndani ya vyama na hatimaye maridhiano baina ya vyama vinavyounda UKAWA, tayari uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Uspika na Naibu Spika umefanyika, kama ifuatavyo;

Katika nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, UKAWA umemteua Ndugu Goodluck Joseph Ole Medeye ambaye atagombea kupitia tiketi ya CHADEMA.

Kwa nafasi ya Naibu Spika, UKAWA watawakilishwa na Ndugu Magdalena Sakaya, ambaye atagombea kwa tiketi ya CUF.


Makene
WAFANYABIASHARA WATISHIWA KUVUNJIWA SOKO WASIPO CHAGUA CCM

WAFANYABIASHARA WATISHIWA KUVUNJIWA SOKO WASIPO CHAGUA CCM

WAFANYABIASHARA mkoani Njombe katika soko kuu wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wa kuichagua Chadema kutokan ana tishilo walilotishiwa aliyekuwa meya wa mji wa Njombe Edwin Mwanzinga wakati akimnadi mgombea utiwani CCM sokoni hapo.

Hayo yalebainishwa katika kampeni za chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na mgombea, chama hicho jimbo la Njombe kusini Emmanuel Masonga alisema kuwa soko hilo ni la serikali na kuwa hakuna anaye weza kulivunja akishindwa uchaguzi.

Masonga aliyasema hayo baada ya kuwepo kwa kauli za kuvunjwa kwa soko kuu la Njombe kama hawata mchagua diwani wa chama cha mapinduzi CCM huku wafanyabiashara wakiachwa midomo wazi.

Alisema kuwa meya huyo hana mamlaka ya kuvunja soko la Njombe mjini na kuwa soko hilo sio la chama kwa kuwa ni soko la mji wa Njombe.

Aliongeza kuwa Wananchi wakiichagua Chadema  kutakuwa na maendeleo katika soko hilo na kukamilisha ujenzi wa mageti katika soko hilo na kuepusha wizi usio wa lazima kutokana na kuto kuwepo kwa mageti sokoni hapo.

Hata hivyo alisema kuwa Haita wezekana mtu aliye shindwa kwenda kuvunja soko kwa kuwa haya kuwa madarakani.

Alisema Chama hicho kitafanya mpango wa kurejesha vitu vyo te vilivyo jengw ana wananchi wakati wa chama kimoja na kumilikishwa CCM na kuwa kama chama kinataka kuwa na mradi kiatakiwa kutumia fedha zake na sio nguvu za wananchi wote katika ujenzi wa mali za vyama.


Alisema hata Chadema wakitaka kuwa ma mradi watarazimika kutumia nguvu zao na sio kutumia nguvu za wananchi katika ukamilishaji wa miradi hiyo.

Kategori

Kategori