JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 17.11.2015.
• MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WILAYA YA RUNGWE AUAWA KWA KUKATWA PANGA.
• MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA ILEA WILAYA YA CHUNYA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA MTI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUSUNGO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EZEKIEL MWALWEGA [34] ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI, MGONGONI NA BEGA LA KULIA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.11.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIPAPA, KATA YA LUFILYO, TARAFA YA BUSOKELO, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI USHABIKI WA KISIASA BAINA YA KIJIJI CHA LUSUNGO NA KIJIJI CHA LUPOTO KATIKA KUGOMBEA NAFASI YA UDIWANI KATA YA LUFILYO.
WATUHUMIWA WANNE WAMEKAMATWA KUHOJIWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI AMBAO NI 1. PAUL MWANDOMBWA [36] MKAZI WA KIFULA 2. IPYANA MWAMAKIMBULA [18] MKAZI WA KIPAPA 3. THOMAS MWASALUKUMO [58] MKAZI WA KIPAPA NA 4. BENJAMIN MWAMBUGA [17] MWANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI LUFILYO KIDATO CHA TATU, MKAZI WA MPULO.
INADAIWA KUWA WATUHUMIWA HAO WANAHUSIKA KATIKA MAUAJI YA MAREHEMU WAKATI AKIWA NA WENZAKE KWENYE GARI MBILI WAKIWA WANATOKA KIJIJI CHA LUPOTO KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KATI YA KIJIJI CHA LUPOTO NA KIJIJI CHAO CHA LUSUNGO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA ILEA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA REMMY UDODI @ JILALA [34] ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA MTI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.11.2015 MAJIRA YA SAA 16:20 JIONI HUKO ILEA KATI, KIJIJI CHA ILEA, KATA YA IFWENKENYA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MTI HUO ULIANGUKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ILIYOKUWA INANYESHA HUKU IKIAMBATANA NA UPEPO MKALI HALI ILIYOPELEKEA MTI KUMUANGUKIA MAREHEMU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZA VULI IKIWA NI PAMOJA NA KUEPUKA KUKAA KARIBU NA MITI MIKUBWA KWANI NI HATARI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.