CCM SABA MBARONI KWA KUGAWA DOZI CHADEMA

WAFUASI watatu wa chama cha deomokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Ludewa wameshambuliwa na watu wanao daiwa kuwa ni wafusai wa chama cha Mapinduzi CCM na jeshi la polisi lina washikiria wafuasi saba kuhusiana na tukio hilo lililotokea usiku wa kuamukia siku ya uchaguzi.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbrod MUtafungwa kusibitisha tukio hilo alisema kuwa jeshi hilo jana liliwakamata na kuwashikili wafuasi saba wa CCM kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuwashambulia wafuasi wa Chadema wilayani Ludewa ambako kumefanyika uchaguzi kumpata mbunge wa jimbo hilo jana.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya jioni katika maeneo ya Lugalawa ambapo haikuwa muda wa kampeni ambapo vijana wanao daiwa ni wafuasi CCM wakiwa kwenye gari yao ambapo vijana wa Chadema walikuwa wanawahoji ni kwanini wapo maeneo hayo wakati muda wa kampeni umepita ndipo walianza kuwashambulia.

"Kwa uchunguzi ambao tumeufanya vijana saba tunao washikili wa CCM walikuwa kwenye gari yao maeneo ya Lugalawa majira ya jioni na muda wa kampeni ulikuwaumeisha walianza kuulizwa na vijana wa Chadema wameenda kufanya nini maeneo hayo ndipo wakaanza kupigwa vijana hao, vijana hao wapo kituo cha polisi wilayani Ludewa kwa kosa la kushambulia Mwili na kudhuru" alisema Mutafungwa.

Alisema kuwa vijana walio jeruhiwa ni vijana watatu wa Chadema huku wawili tayari wameruhusiwa na mmoja bado yopo katika hospitali ya Lugalawa ambaye amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwa ni pamoja na kichwani na vitu vyenye ncha kali.

Hata hivyo makamu mwenyekiti wa Bavicha taifa, Patric Ole Sosopi anasema kuwa vijana hao walijeruhiwa vibaya na kuwa ni kweli ni wafuasi wa chama hicho.

Alisema kuwa watu walioumizwa ni watano na kuwa wawili wamelazwa hospitali ya Lugalawa na kuwa mmoja alipo pigwa na wafuasi wa CCM waliamua kumpeleka wao wenyewe katika kituo cha polisi ambapo kijana huyo alipigwa maeneo ya mlangani na kuwa baada ya matukio hayo pia vijana hao walipita katika maeneo la Mawengi, Mlangali na kupiga wafuasi  chama hicho.

Alisema kuwa vijana hao wa CCM walikuwa na gari yenyi namba ya usajili T 155 CKS  na kuwa waliikamata gari hiyo na kuipileka katika kituo cha polisi.

Hata hivyo CCM wamekili kukamatwa kwa vijana wao ambao mpaka kufiki majira ya saa 9:00 Mchana walikuwa mado wanashikiliwa na jeshi hilo.

Akizungumzia kukamatwa kwa vijana wao katibu wa CCM wilaya ya Ludewa, Lusiana Mbosa, kulitokea mapambano kati ya vijana wao na vijana wa Chadema wakati mgombea  ubunge akiingia katika eneo la Lugalawa ambapo vijana wa ulinzi wa CCM Greenguard walikuwa dolia maeneo ya Lugalawa.

Alisema kuwa walipo kutana vijana walio kuwa wakimlinda mgombea wa Chadema, Bathromeo Msambishaka, wakaanza mapambano ambapo ilibainika kuwa kuna hujuma ambazo zilitaka kufanyika katika maeneo hayo ya kijiji cha Lugalawa.

 Alisema kuwa vijana hao wakati wakipambana ni vijana wa Greenguad na Redbriguad ambapo vijana wa CCM walibaini kuwa mbunge anataka kufanya hujuma za uchaguzi ambao ulitakiw akufanyika jana.

Hata hivyo mgombea ubunge anaye tuhumiwa kutaka kufanya hujuma na Mwenyekiti wa CCM, amesema kuwa gali ya CCM aina ya Hadtop ilifika katika eneo la Lugalawa ambapo walikuwepo baada ya kumaliza kampeni zao walianza kuvamiw ana vijana wa CCM walio toka katika gari hiyo kabla ya kuwateka watu wawili wa Chadema.

Msambichaka ameongeza kuwa walipowakamata walianza kuwapiga na kuwa meneja kampeni wake naye alikamatwa na kuwa kuna watu walipigwa vichwani na vitu kama chuma  na kuwa mtu mmoja alipigwa mpaka alidondoka chini.

Hata hivyo Msambishaka alitaja majina ya walio jeruhiwa kuwa ni Focas Mtitu ambaye alipigwa kichwani na kujeruhiuwa vibaya na Seba, alitibiwa na kuruhusiwa, Geogina alipigwa na kukimbi huku siku ya jana jioni kurejea, na mmoja aitwae Lenard mpaka sasa hajulikani aliko na kuwa msichana mmoja alibakwa katika tukio hilo baada ya kupigwa.