Mmoja azaliwa Njombe

USIKU wa kuamkia siku ya Krismasi amezaliwa mtoto mmoja wa kiume katika hospitali ya mkoa wa Njombe Kibena.

Akizungumza na ELIMTAA mkoani Njombe muuguzi wa zamu katika hospitali ya mkoa wa Njombe Kibena Emmy Mbela jana alisema kuwa mtoto huyo alizaliwa usiku wa Disemba 25  katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa katika hospitari hiyo amezaliwa mtoto mmoja majira ya
saa 7:30 usiku ambapo kabla ya kufika majira ya saa 6:00 usiku wa Disemba 25 walizaliwa watoto na majira ya alfajili kuna watoto pia walizaliwa.

Muuguzi Mbela alisema kuwa licha ya kuzaliwa kwa mtoto huyo mmoja
usiku wa krismas kabla ya hapo watoto walizaliwa na asubuhi ya jana
watoto waliendelea kuzaliwa ambapo mpaka ELIMTAA inaondoka Hopitalini hapo watoto 3 walikuwa wamezaliwa alfajili.

Aidha kwa upande wa jeshi la polisi mkoani Njombe liliimarisha ulinzi katika mji wa Njombe na usiku huo kupita bila kuwapo kwa tukio lolote la uvunjifu wa amani.

Akizungumza na ELIMTAA kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani alisema kuwa mkoa kwa usiku wa mkesha wa Krismasi ulienda vizuri bila ya kuwapo kwa tukio lolote la kiharifu wala ajari.

"Mkoa upo shwari na usiku kucha hakuna tukio lolote lililotokea na tunaendelea kuimalisha ulinzi siku ya leo katika sehemu zte zenye mikusanyiko ya watu hapa mjini," alisema Ngonyani