WATOA MIMBA WAONYA, HUENDA WANATUPA VIONGOZI WA KESHO

WAKRISTO kote nchini wametakiwa kujihadhari na mimba zisizo tarajiwa na kuzitoa kitu ambacho wanakinyima haki kiumbe hicho ambachi kingezaliwa huenda kingukuwa Rais, au mkombozi wa taifaletu na ufisadi mbalimbali ukiwemo wa Escrow na ubadhilifu mbalimbali.
 Akuhubiri katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi ambayo inaazimishwa duniani kote ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Mseminali wa kanisa katiriki la Njombe mjini, Bosco Mligo, alisema kuwa watu wanao toa mimba wanaua viongozi ambao baadae wangeweza kuliokoa taifa letu.
 Alisema kuwa kama kutoa mimba zinazo patikana nyumbani ang’ekuwa wa kwanza Mariam ambaye alipata mimba akiwa nyumbani kwao na akiwa katika hatua za uchumba na Yusufu.
 Alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiogopa kudhalilika kwa kupata mimba wakati wakiwa nyumbani kwao na kuanza kuitoa kitu ambacho wanatoa viongozi ambao ni watu muhimu katika taifa na ulimwengu.
 Alisema Mariam kama angetoa mimba aliyo ipata kwa uweza wa roho mtakatifu angekuwa amemtoa mwokozi wa wakristo ambaye alitabiliwa katika vitabu vitakatrifu miaka mingi kabra ya kuzaliwa kwake.
 Mligo alisema kuwa watu wamekuwa wakifurahia wakati wa tendo la ndoa lakini matokeo ya tendo hilo wamekuwa wakilichukia.
 Alisema kuwa watu wamekuwa wakijua matokeo ya tendo hilo lakini matukeo yake yamekuwa ji magumu kupokelewa, alisema kuwa vitendo hivyo vya utoaji mimba vimekuwa vikiwaathiri watu wengi kisaikorojia.
 “Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na watu wengi ambao wanaonekana kuwa kama wamechanganyikiwa hiyo wengi wao inasababisha na utoaji wa mimba kitu ambacho watoto walio watoa wanawalilia na kuwachanganya akili,” alisema Mrigo.
 Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakifanya vitendoi hivyo kutoka na kukataliwa ama kuto kuwa na roho wa Mungu juu yao na kuwa na moyo mwepesi.
*********************************************
CONTACT WITH ELIMTAA BLOG BY: CALL :+255 753 321191  EMAIL: furahanews1@gmail.com Facebook: www.facebook.com/elimtaa Twitter: www.twitter.com/@elimtaa "ANY TIME CALL US FOR ADVERTISEMENT, OR ANY NEWS YOU WANT APPEAR TO Elimtaa Blog" Elimtaa 'more news update your mind'