Madereva wanyimwa dhamana kwa tuhuma za wizi

DEREVA mmoja wa kampuni ya Lake Oil na abiria wake wawili
wamepandishwa mahakamani jana kwa tuhuma za kuiba sahani ya shaba,
katika mahakama ya wilaya ya Njombe mkoani hapa na kunyimwa dhamana
mpaka mahakama ipitie maombi ya dhamana yao ambayo yamewekewa
pingamizi na upande wa jeshi la polisi..

Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani kwa  mara ya kwanza  Januari 8,na
kusomewa maelezo ya awali katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya
Njombe, mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,  John Kapokoro,
mwendesha mashitaka wa serikali Riziki Matiku alisema kuwa washitakiwa
walitenda kosa hilo Disamba 10 mwaka jana.

Alisema kuwa washitakiwa hao Deocles Deus, Joshua Chamhene na Jacob
Yohana walitenda kosa hilo Desemba 10 mwaka jana, ambapo wanadaiwa
kuiba sahani ya shaba mali ya kampuni  tajwa ambayo ni mwajili wa
Mshtakiwa namba moja , na kukamatwa na jeshi la polisi na kupatiwa
ambapo walikaa rumande kwa siku sita pasipo kufikishwa mahakamani na
kisha kupata dhamani kabla ya kufikishwa kizimbani.

Matiku aliiambia mahakama kuwa wamepata kiapo cha kuzuia dhamana ya
washitakiwa kutoka kwa afisa wa polisi, Joseph Kate kwa lengo la kuto
haribu taratibu za upelelezi wa kesi hiyo ambayo inadaiwa kuwa kuna
watuhumiwa wengine bado hawajakamatwa na upelelezi bado unaendelea.

Kwa upande wa wakili msomi wa washitakiwa hao Gabriel Malangalila
alisema kuwa ni kinyume cha sheria kuwanyima dhamana washitakiwa kwani
sheria inasema kuwa kila mtu anahaki ya kupata dhamana kama atatimiza
mashalti ya dhamana ikizingatiwa kuwa mshtakiwa anatakiwa kupatiwa
matibabu kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa wafanyakazi wa
kampuni hiyo ambao hata hivyo hawakutajwa.

Alihiji sababu za  washitakiwa kunyimwa dhamana ili hali awali wakiwa
kituo cha polisi makambako walipatiwa dhamana na Polisi kwanini
mahakamani wanyimwe dhamana akajaribu kuishawishi mahakama hiyo
kutotekeleza pingamizi hilo na kutaka sheria  isipindishe sheria kwa
kuwanyima dhamana washitakiwa hao kwa kusikiliza maombi ya upande wa
mashitaka hata hivyo haikusaidia.

Baada ya upande wa utetezi tutoa hoja zao upande wa mashitaka nao
ulisema kuwa wakili  msomi Malangalila kwa kuwa hakutaja kifungu
kitakacho vunjwa baada ya kuwanyima dhamana alisema kuwa upande wake
unaomba dhamana hiyo isitolewe na mahakama kutokana na kulina taratibu
za kiupelelezi.

 "Mheshimiwa hakimu naomba wateja wangu wapatiwe dhamana
ili wakaendelee na matibabu kwani mshitakiwa mmoja anasindano mkononi
ambayo aliwekewa drip hospitalini," mahakama awali ipipanga kutolewa
uamuzi wa kutolewa dhamana ama kukataliwa Januari 21Hakimu: "Dhamana
itatolewa baada ya kupitia maelezo yenu Januari 21
"alisema.

"Utaratibu utafanyika  washitakiwa kama wanaumwa watapelekwa
husipitalini na magereza
wakati wanasubilia ruling ya mahakama hii, .........  Okey kwa sababu mmeomba
kupunguziwa muda wa kupata ruling ya kupata dhamana ama lah basi
januali 19 mje nitakuwa na maamuzi juu ya pingamizi washitakiwa
wataenda mahabusu mpaka tarehe hiyo,"alisema mh. Hakimu.

Upande wa utetezi uliiomba mahakama kutoa  wapangia muda mrefu wa
kutolewa kwa maamuzi licha ya kunyimwa dhamana hiyo ambayo ni haki ya
wateja wake.