MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kamati ya
maudhui imeanza ziarayake mkoani Mbeya katembelea vituo vya radio ili kupitia
maudui ya Vituo hivyo kwa lengo la kuboresha matangazo.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati hiyo
Eng. Magret Mnyagi alisema kuwa lengo la ziara hiyo katika vituo vya radio
Mkoani Mbeya ni kuangalia maudhui ya Vituo vya Radio na kuangalia jinsio gani
ya kuboresha matangazo ya radio kwa faida ya mlaji wa habari.
Alisema ziara hiyo ni ya siku Mbili mkoani Mbeya na
itahusisha vituo vyote vya radio mkoani humo na kuzungumza na watangazaji wa
vituo hivyo ili kujua changamozo zinazo wakabili watanzazaji na kuhakikisha
matangazo yanayo ruka yanakuwa yenye maudhui mazuri.
Eng. Manyagi alisema vitu watakavyo viangalia ni pamoja na
matumizi ya Lugha na mikataba ya watumishi katika vituo hivyo ambavyo
inasadikika wanatumiwa watu wasio na elimu ya Uandishi wa habari na Utangazaji.
Alisema kuwa kukupitia ziara hii itapanua umakini wa
watangazaji katika matumizi ya lugha kwa watangazaji hivyo lugha sanifu
itatumika kufikisha ujumbe kwa jamii.
Eng. Manyagi alisema watawakumbusha na kuwafundisha wale
ambao hawazijui kanuni za utangazaji ili kuwaepusha watangazaji kuingiza mambo
ya uchochezi kupitia vyombo vya habari.
Alisema ziara hii imeanza mapema huku nchi ikielekea kwenye
miaka ya uchaguzi mkuu ambao unakua wa mambo mengi ya kisiasa.
“Tumeanza mapema tukijipanga kuelekea uchaguzi mkuu ambao
umekuwa na mambo mengi na baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakizinunua baadhi ya
Radio na kuto waruhusu wengune chombo cha habari kinatakuwa kuwa huru na
kutangaza habari za vyama vyote,” alisema Eng. Manyagi