Kufuatia kuwakamata wanawake 38 nchini Tanzania,kwa kuwafanyia ukeketaji
haramu kundi la wasichana wa mji wa Same, wanaharakati wamelipokea
suala hilo kwa mtazamo tofauti, wakitaka sheria ifanye kazi.
Wanawake hao walikamatwa wakati wakicheza ngoma za asili katika nyumba
moja, ambako polisi iliwakuta wasichana 21 wenye umri kuanzia miaka
mitatu hadi 15, waliokwisha keketwa. Flora Nzema amezungumza na Jovita
Mlay mwanaharakati wa masuala ya ukeketaji, ambaye kwanza anaelezea
namna alivyoipokea hatua ya kuwafikisha wahusika mahakamani. Je
kufikishwa mahakamani kwa wanaoounga mkono vitendo vya ukeketaji
kutasaidia kukomesha vitendo hivyo nchini Tanzania?Na Dw.de