KUFUATIA kuwapo kwa upungufu wa wataalamu na wakandarasi
kwenye mafuta na gesi hapa nchini chuo kikuu cha sayansi na techniloji (Must)
kimetakiwa kuanzisha mafuzo yanayo husu mafuta ili nchi kutochukua wataalamu
kutoka nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Makame Mbarawa wakati wa maafari ya kwanza ya chuo kikuu cha Sayansi
Mbeya.
Prof. Mbarawa alisema kuwa kufuatia kuwapo kwa uhitaji
mkubwa wawataalamu katika madini ya mafuta na Gesi kunahaja ya chuo Kikuu hicho
kuanzisha mafuzo ya nayo husiana na uchimbaji wa gesi na mafuta.
Alisema kuwa kuwapo kwa masoma yatakayo watoa wataalamu wa
uchumbaji wa Mafuta na Gesi, nchi itaipunguza gharama za kuwagharamia wataalamu
wa uchimbaji kuja kufanya kazi hizo.
“Kuna umuhimu wa kuanzisha masomo yanayo husiana na uchumbaji wa gesi kwani tukiwa na wataalamu kutoka hapa nchini serikali itapunguza gharama za kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchii” Alisema Prof. Mbarawa.
Alisema serikali
itapunguza gharama kubwa ambazo itaziingia hivi karibuni wakati haina wataalamu
wa kutosha kuchimba gesi kwa kuakiza wataalamu kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wa ke makamu mkuu wa chuo Kikuu cha Must Joseph
Msambichaka alisema chuo hicho kinafya jitihada za kuhakikisha wataalamu wanao
toka katika chuo hicho wanaisaidia nchi kutoka na utaalamu wanaupata chuoni
hapo.
Hivyo alisema kuwa chuo hicho kitakuwa msaada kwa nchi kwa
kuzalisha wataalamu ambao watakuwa msaada katika mambo malimbali hapa nchini
ambayo yatahitaji utaalamu.
Chuo hicho ambacho awali kilikuwa kikiitwa
taasisi ya Sayansi Mbeya (Mist) sasa Kimepandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu cha
Sayansi Mbeya (Must) toka kimepandishwa hadhi sasa ni mara ya kwanza kuzalisha
wataalamu wa sayansi, kupandishwa hadhi huko kulitabiliwa na mwalimu Julius Nyerere
alipo tembelea chuo hicho enzi za uhai wake