Vikosi vya Somalia sasa vinampekua kila mtu, wakiwemo raia wa kigeni, wanaotembelea majengo ya serikali na shughuli katika maeneo ya umma yanayohusisha protokoli za usalama za serikali.
Awali, wageni, hasa watu wa Magharibi na Wazungu, walikuwa wanaachiwa katika upekuzi wa kiusalama za watu tafauti waliohuhudhuria, wakati raia wa Somalia walikuwa wanapekuliwa.
Lakini kuanzia mwanzoni mwa Desemba, vikosi vya usalama vilianza kuendesha upekuzi wa kiusalama bila ya kubagua, naibu mkuu wa usalama kwa mkoa wa Benadir Warsame Mohammed Jodah aliiambia Sabahi.
"Tumeagiza askari wa usalama kumekua mtu yeyote awe ni mgeni au mwenyeji ili kuhakikisha usalama, kitu ambacho ni muhimu sana kwetu sote," Jodah alisema.
Hoja ya utekelezaji wa upekuzi wa usalama bila ubaguzi haukuja kufuatia kukamatwa kwa raia wa kigeni au tukio jengine lolote, Jodah alisema, bali lilikuja wakati maafisa kupitia upya itifaki ya usalama walipoona walikuwa wakitoa ushughulikiaji maalum kwa mashirika yasiyo ya Kisomali kwa heshima.
"Kinachoendelea ni kwamba mgeni ambaye hapekuliwi anaweza kuingia katika eneo lolote kwa shughuli ya aina yoyote," alisema.
Al-Shabaab wanayo mafungamano na mitandao ya kigaidi ya kimataifa na inawatumia watu wa mataifa tofauti ili kufanya mashambulizi, alisema, na "ndio maana hatutaki kuwapa magaidi fursa".
"Kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria, ningewashauri raia wa kigeni wawe na subira ikiwa watatumia saa nyingi katika operesheni za usalama wakati kila mtu anapopekuliwa," alisema.
Taratibu mpya za usalama zapingwa na baadhi
Mohyadin Sirad Isaq, mwenye umri wa miaka 29, mlinzi wa usalama katika majengo ya mahakama ya mkoa wa Benadir, karibuni alikumbana na matatizo wakati alipowaomba Wazungu wawili kuwapekuwa walipotaka kuingia mahakamani.
"Jukumu letu ni kumpekua kila mtu anayetaka kuingia mahakamani, iwe ni Msomali au mgeni," alisema. "Tuliwaambia, 'ni jukumu letu kukupekueni, na tungewaomba kwa heshima mkubaliane na upekuzi huu."
"Hata hivyo, mara nyingine tunakuwa na kutoelewana na wakalimani wa Kisomali ambao hawataki wageni weupe waliofuatana nao wasipekuliwe kwa sababu hawafamu [umuhimu wake]," aliiambia Sabahi. "Lakini tunaamini kwamba ni lazima kwa usalama wa kila mtu."
Isaq alisema aliingia katika malumbano tarehe 10 Desemba na mkalimani wa Kisomali aliyekuwa anaongozana na waandishi wa habari wa kigeni waliokuwa wanatembelea mahakama ya mkoa ya Benadir.
"Wakati nilipotaka kupekua mikoba yao ili kufanya upekuzi wa kina, mkalimani wa Kisomali aliniambia kuwa nisiwapekue watu hawa kwa sababu ni watu weupe ambao hawana chochote tunachotafuta," alisema.
Isaq alimweleza kwamba pekuzi hizi zilikuwa sehemu za upekuzi wa usalama wa kawaida na dhamiri yake haikuwa kuwapekuwa watuhumiwa tu, lakini mkalimani hakufahamu.
"Malumbano yetu yalikua na kuwafika wakubwa wangu," alisema. "Hatimaye niligundua kuwa watu wale aliokuwa nao walikuwa waandishi wa habari kutoka nje, lakini hakuna njia kwangu mimi ya kumjua mgeni ambaye uso wake ni mgeni kwangu. Kamanda wangu alinisifia kwa kuwa imara katika usalama."
Sahra Yusuf, mwenye umri wa miaka 27 ambaye alisoma masuala ya uongozi na biashara katika Chuo Kikuu cha Simad, alikaribisha uamuzi huo wa kuzidisha pekuzi za usalama.
"Ni mafanikio mazuri kwamba wakati upekuzi unapofanyika, hakuna mtu anayepata ushughulikiaji wa kipekee," aliiambia Sabahi. "Ndio maana ninaamini kwamba tunaweza kuwashinda magaidi wanaotumia vitambulisho tofauti ili kutuua. Tunapaswa kuwa na tahadhari kwamba raia wa kigeni ni sehemu ya operesheni za silaha kutumia za al-Shabaab. Watu hawa wanapaswa kuzuiwa katika kujifumba wenyewe."
Na Sabahi Online