Sanamu ya rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela imezinduliwa
mjini Pretoria.
Sanamu hiyo imezinduliwa baada ya mazishi ya kiongozi huyo
kwenye kijiji cha Qunu, siku ya Jumapili na siku kumi za maombolezo ya
kitaifa.
Mandela alifariki dunia tarehe 5 ya mwezi huu wa Disemba baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Uzinduzi huo umeenda sambamba na siku ya
maridhiano ya Afrika Kusini. Akizungumza wakati wa sherehe hizo katika
majengo ya Muungano, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alisema sanamu
hiyo ni ishara inayotoa wito kwa watu kuungana pamoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
sana