Sanamu ya Mandela yazinduliwa

Sanamu ya rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela imezinduliwa mjini Pretoria. 
Sanamu hiyo imezinduliwa baada ya mazishi ya kiongozi huyo kwenye kijiji cha Qunu, siku ya Jumapili na siku kumi za maombolezo ya kitaifa. 
Mandela alifariki dunia tarehe 5 ya mwezi huu wa Disemba baada ya kuugua kwa muda mrefu. 
Uzinduzi huo umeenda sambamba na siku ya maridhiano ya Afrika Kusini. Akizungumza wakati wa sherehe hizo katika majengo ya Muungano, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alisema sanamu hiyo ni ishara inayotoa wito kwa watu kuungana pamoja.