SERIKALI imetoa udhamini wa masomo (Scholarship) kwa Mwanachuo mmoja aliyehitimu masomo ya shahada ya Umeme katika Chuo kikuu cha Sayansi Mbeya University of Technology and Science (Must) baada ya kufanya vizuri katika masomo yake ya Umeme.
Mgeni Rasmi Waziri wa mawasiliano na Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akimpa hongera mwanafunzi bora Lilian Kawala.
Udhamini wa huo wa kwenda Kusoma Masta ya Umeme, ulitolewa kwa Lilian Kalawa na Waziri wa Mawasiliano na Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa alisema Serikali imetolewa ili kuhakikisha teknolojia inakua hapa nchini kwa kupata wasomi wengi.
Alisema kuwa serikali itaendelea kutoa ufadhiri kwa wanafunzi watakao fanya vizuri masomo ya sayansi hapa nchini ili kupata wanawake wengi katika fani ya sayansi.
Prof.Mbarawa alisema kuwa serikali itatoa ufadhili kwa wanafunzi kusoma bure katika elimu zao za juu na kuhakikisha nchi inakuwa na wanawake wataalam wenye masta.
Alisema kuwa Kalawa atasoma masta bure kwa udhammini wa serikali ambapo kitakapo patikana chuo atakacho kwenda kusoma mwezi wa Septemba mwaka ujao ili kupata wanawake wengi wenye elimu ya juu upande bwa sayansi.
Hivyo alisema kuwa Mwezi Septemba ataenda kusoma masta yake nje ya nchi ili kuondeza elimu yake kama atakuwa tayari na serikali italipia masomo yake yote.
Kwa upande wake Kalawa alisema kuwa kufikia hatua hiyo ya kuongoza ni juhudi alizo zifaya katika masomo yake na kuwa atasoma kwa bidii katika masomoyake na kuitumia fulsa hiyo ya kusomeshwa na serikali.
Alisema atafanya juhudi katika masomo yake ili kuhakikisha anafanya vizuri akiwa masomoni nje ya nchi na kuhakikisha aiangushi serikali.
Aliongeza kuwa mpaka anapata nafasi hiyo amepitia katika vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudhalauliwa na watu mbalimbali ambao wanasema wanawake hawawezi.