JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
|
TAARIFA
KWA UMMA
UTEUZI
WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amemteua Prof. Penina Mlama kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria
ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 na hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10
Desemba, 2013.
Aidha, kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo,
Prof. Makame M. Mbarawa (Mb), Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, ambaye kwa mujibu wa hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya na mamlaka aliyonayo amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Baraza
la Chuo:
1. Mhe.
Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Viti Maalum-Njombe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
na Sheria, Mwakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
2. Eng.
Peter Chisawilo, Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo, Mjumbe
wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Mwakilishi wa Sekta Binafsi;
3. Dkt.
Haji Mwevura Haji, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Chuo Kikuu cha Taifa
Zanzibar, Mwakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
4. Bw.
Bernard T. D. Mbonde, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi
na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia Mbeya;
5. Prof.
Evelyne Mbede, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia;
6. Bw.
Mapunda Erick Chrisantus, Mhadhiri na Rais wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Chama cha Wahadhiri wa
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya; na
7. Bw.
Augustine K. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera za Uchumi Mpana, Mwakilishi wa
Wizara ya Fedha.
Uteuzi
wa wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni wa
kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.
Imetolewa
na;
Prof.
Patrick J. Makungu,
Katibu Mkuu,
NA MBEYA YETU