APIGWA MAWE MPAKA KUFA



MKAZI wa kijiji cha Lema kata ya Ngana wilayani Kyela mkoani Mbeya, Bicco Mwakibibi ameuwawa kwa kupigwa na mawe na wananchi baada ya kutuhumiwa kuwa ni mwizi.

Kananda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa katika kijiji cha Lema kata ya Ngana wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Alisema marehemu alipihwa na mawe, Fimbo pamoja na silaha za jadi baada kumtuhumu kuwa ni mwizi.

Msangi amesema kuwa Mwakibibi alipigwa na weananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kusababisha kifo chake.

Akisimulia tukio hilo msangi alisema kuwa marehemu akiwa na mwenzake kabla ya kuuwawa walivunja kibanda cha biashara na kuiba.

Alisema mwenzaka alikimbia baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta zinafanywa na jeshi la Polisi.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.

Msangi ametoa wito kwa jamii kuto jihusisha na tabia za kujichukulia sheria mkononi na kusababisha vifo kwa watuhumiwa na badalayake wawachukue na kuwafikisha katika vyombo vya sheria na kuiachia sheria kuchukua nafasi yake.