JESHI
la Polisi Mkoa wa Mbeya lina mtafuta, Bonny Silumbe Mkazi wa kijiji cha Kapele
wilayani Momba Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumchoma kakayake kisu cha mgongoni.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Polisi Mbeya,
Ahmed Msangi (Pichani), amesema kuwa tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kapele
wilayani Momba juzi majira ya saa 3:00 Usiku.
Alimtaja marehemu huyo aliyekufa wakati akipatiwa matibabu
katika Hospitali ya wilaya ya Mbozi baada ya kuchomwa kisu cha mgongo na Mdogo
wake kuwa ni Adamu Silumbe.
Akisimulia tukio hilo Msangi alisema kuwa marehemu alichomwa
kisu cha mgongoni baada ya marehemu kutangaza kuwa marehemu alimtorosha mke wa
mtu kijijini hapo.
Alisema mtuhumiwa alitenda tukio hilo akiwa na lengo la kulipiza
kisasi kwa kaka yake.
Mtuhumiwa alitoroka mda mfupi baada ya kutenda tukio hilo na
jeshi la polisi lina mtafuta ili kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Alisema mwili wa marehemu ulikabishiwa kwa ndugu ili kufanyika
taratibu za mazishi.
Alisema kuwa wanandugu walitakiwa kukete meza moja na kujadili
na sikama alivyofanya mtuhumiwa.