Kiasi ya wanajeshi 66 wameuwawa katika mapigano kwa muda wa siku mbili zilizopita katika mji mkuu wa Sudan kusini Juba.
Daktari katika hospitali ya jeshi Ajak Bullen amesema kuwa hadi sasa jeshi limepoteza wanajeshi saba ambao wamefariki wakati wakisubiri kupata matibabu na wengine 59 wameuwawa katika mapambano.
Hospitali nyingine mjini Juba , ambayo ni hospitali ya kutoa mafunzo kwa madaktari, imeripoti hapo kabla watu 28 wamefariki, ikiwa ni mchanganyiko wa wanajeshi na raia.
Msemaji wa jeshi Philip Aguer amekataa kusema lolote juu ya idadi ya watu waliofariki, akiliambia tu shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi wanadhibiti hali hivi sasa.Wakati huo huo milio ya hapa na pale ya risasi iliendelea kusikika katika mji wa Juba, wakati wanajeshi wanaendelea na zoezi la kupambana na mabaki ya kundi la wanajeshi wanaotuhumiwa kufanya jaribio la mapinduzi.
Na Dw.de