SHULE ya
msingi Makambako ya halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe, wamekabiziwa
madarasa mawili na ofisi kukiwa na madawati 50 katika madarasa hayo huku shule
hiyo ikikabiliwa na upungufu madarasa na kusababisa wanafunzi kujazana katika
madarasa.
Shule hiyo
inamlundikano wa wanafunzi ukitofautisha na madarasa yaliyopo katika shule hiyo
ambayo ipo katikati ya mji mkubwa kuliko yote mkoani Njombe.
Akipokea
madawati hayo mkuu wa shule ya Makambako inaupungufu wa vyumba vya madarasa 24
ambapo watoto wa darasa la kwanza na lapili wamekuwa wakisoma kwa zam huku idadi
ya waalimu ikiwa ni ileile.
Mwalimu huyo
amepokea amepokea Madarasa na madawati kutoka Benki ya Posta Tanzania ambayo
imewajengea Madarasa hayo kwa thamani ya Milioni 19 pamoja na madawati.
Mkuu wa mkoa
wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi anakuwa ni mgeni Rasimi wakati wa kupokea dawati
na vyumba hivyo vilivyo kabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta, Letisia
Lutashobya.
Shule hiyo
inakabiliwa na upungufu wa vyumba hivyo kutokana na kuwapo kwa elimu bule
kunako sababisha wanafunzi wengi kujitokeza kusoma.