HALMASHAURI
ya Mji wa makambako mkoani Njombe, inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo za kiuendeshaji tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2013.
Hayo
yamebainishwa katika kikao cha cha baraza la madiwani ambapo imebainika kuwa
imeshuka kimapato uwezo wa kujitegemea umepungua kutoka asilimia 18 kujitegemea
na sasa imeshuka hadi asilimia 15.
Akiwasilisha
taarifa katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Chesco Mfikwa,
amekiri kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji na kwamba inatokana na baadhi
ya wafanyabiashara kugoma kutumia mashine za kielektroniki (EFD).
Akimwakilisha
mkuu wa Mkoa katika kikao hicho Katibu wa Tawala wa Mkoa Jacson Saitabahu
anatoa ushauri kwa madiwani kutoka hapo walipo
hivi sasa.
Deogtius
Peter Mkaguzi mkazi wan je wa mkoa wa Njombe, akatoa ushauri ili kukabiliana na changamoto hizo.
Angalizo
likatolewa kwa watendaji kuhakikisha elimu inatolewa kwa wafanya biashara
kuhakikisha watumia mashine za EFD ili kuepukana na ukwepaji wa kodi nakwamba
sio hiari ni amri ya serikali na hivyo linahitaji utekelezaji.