Makamishina waapishwa


MAKAMISHINA wa skauti wilaya za mkoa wa Njombe wametakiwa kutengeneza mikakati wa kimaendeleo na kuiwasilisha kwa wakuu wa wilaya ili kuitekeleza na kuwainua vijana walioko skauti katika wilaya.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe, Dr. Rehema Nchimbi wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha makamishina wa wilaya wa skauti kwa mkoa wa Njombe iliyofanyika juzi mkoani hapa.

Dr. Nchimbi alisema kuwa makamishina wa skauti wa wilaya ambao baadhi yao ni waalimu wa shule katika wilaya hisika waandae mipangop mikakati ya kimaendeleo na kuiwasilisha wa walezi wa skauti wa wilaya ambao ni wakuu wa wilaya na kuifikisha wa wakulegenzi kwaajili ya utekelezaji.

Alisema kuwa kwa kuwa Rais  wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania ni mlezi wa skauti wa taifa na wakuu wa mikoa ni walezi wa mkoa na kuwa basi wakuu wa wilaya ni walezi wa skauti wa wilaya.

Alisema kuwa mipango hiyo ya kimaendeleo wanayo takiwa kuiibua ni pamoja na miradi ya upandaji wa miti ambapo wakiandaa mipango yao waipeleke kwa mkuu wa wilaya na kuwa miradi hiyo itawasaidia skauti kujiendeleza kielemu na kuwasaidia pale wanapo kwama wanapo taka kutekeleza miradi yao.

Hafla hiyo ilishuhudiwa na skauti kutoka halmashgauri ya Makambako, Wanging’ombe na Njombe, ambapo alikuwepo na kamishna wa skauti mkoa wa Njombe ambaye alisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi wanapo hitaji kuendesha shughuli zao.

Kamisihna Tutsiwene Mahenge alisema kuwa katika uendeshaji wa skauti kwa mkoa wa Njombe umekuwa ukikwama kutokana na kuto kuwa na pesa na kuwa licha ya kuto kuw ana pesa za kutosha kufika katika kila kona ya mkoa wa Njombe wamefanikiwa kuwafundisha vijana wa skauti 3,000 kwa mkoa wa Njombe kutoka shule za sekondari na msingi.

Alisema kuwa skauti katika mkoa huo ilikufa na kufufuka tena mwaka 2009 ambapo wakati inafufuliwa kulikuw ana shule moja tu ambayo ilikuw an skauti kwa mkoa wa Njombe ambapo baadhi ya shule zilikuwa na skauti ambayo haija sajiliwa.

Alisema kuwa wamefanikiwa kupata wakufunzi katika shule mbalimbali mkoani Njombe wapatao 80 ambao wameendelea kuwafundisha vijana hao na kuifanya skauti kuimarika mkoani hapo.


Alisema kuwa skauti ni ukakamavu na kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo ya ukamamavu na kung fu kwa wanafunzio hao na kuwa mafunzoi hayo yamekuwa yakitolewa kwa lengo la kujenga kizazi chenye ukakamavu na si kwaajili ya ugovi.