WAFANYABIASHARA ya
usafirishaji pikipiki maarufu bodaboda mkoani Njombe wamekama na jeshi la
polisi kwa kile kinachodaiwa wamefanya vurugu na kuchoma gari lililo sababisha
ajali na kifo cha dereva wa pikipiki.
Jeshi la polisi linaendesha msako wa kukamata waendesha
bodaboda kwa siku ya tatu jana kwa lengo la kuchambua walio husika na tukio
hilo huku walio kuwemo na wasio kuwemo kukamatwa wao pamoja na pikipiki zao.
Akizungumzia suala la
kamatakamata hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani amesema
kuwa jeshi hilo linaendesha msako wa kuwakamata madeleva wa bodaboda kwa lengo
la kuwabaini wale walo husika na matukio mawili ya kuchoma hali na kuvamia
polisi na kuwarushia mawe.
“Taarifa za interijensia
zinasema kuwa watu zaidi ya 200 walihusika katika tukio la kuvamia polisi
waliokuwa wamekamata wezi wa pikipiki na tutaendelea kuwawaka mpaka tukakikishe
walio husika na wengine wale waliohusika na uchomaji wa gari lililosababisha
ajali lililokuwa na zaidi ya thamani ya shilingi milioni 34,” alisema Ngonyani.
Aidha kwa mujibu wa Kamanda
wa polisi alisema kuwa wamekamata madereva bodaboda 18 na kuwa jeshi hilo
linaendelea na kuwatafuta wengine na kuwa jeshi la polisi halijazuia biashara
hiyo kuendelea licha ya kuwa vituo vyote vya bodaboda havina pikipiki na habari
kutoka kwa vyanzo visivyo aminika zinasema kuwa watu zaidi ya 120 wanashikiliwa
na jeshi la polisi.
Kwa upande wa madereva
wa pikipiki wamelalamikia kitendo kinacho fanywa na jeshi hilo kwa kuwa kinakamata
watu bila kujua ni dereva ama sio derevava.
Wakizungumza bila
kutaja majina yao walisema: “Polisi sasa wanatunyanyasa hata ambao hatukuhusika
kwani wakikukuta barabarani bila kukuuliuza wanakukamata na kukunyanganya
pikipiki na ukikimbia wanakokopa pikipiki,” alisema Dereva huyo.
Alisema kuwa
wanapokutwa njiani wanawakamata na kuwapiga virungu na kasha kuwanyang’anya
pikipiki zao.
Alisema kuwa kuma mzee
kutoka kijijini alikamatwa baada ya kukutwa akiwa katika kituo cha bodaboda
akimsubiri dereva wa bodaboda ili ampeleke nyumbani baada ya kutoka vijijini.
Nae mwenyekiti wa
madereva bodaboda Philimon Mwinuka alisema kuwa kitendo kinacho fanywa na jeshi
la polisi ni uonevu na kuwa wanawanyima haki watuiaji wa usafiri huo kwa kuwa
hakuna dereva anaye fanya biashara hiyo kwa zaidi ya masaa 48 tangu kuanzishwa
kwa oparationi hiyo kwa kuwa wakiingia barabarani wanakutana na polisi wanao
kamata bila kuulizwa.
Alisema kuwa jeshi la
polisi lilitakiwa kuhakikisha wanakaa na uongozi wa wa bodaboda ili wawatajie
walio husika kwaniu wanafahamiana kuliko kitendo kilicho fanywa na jeshi la
Polisi.