MKUU wa mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi wamewataka wadau wa ukuzaji na uendelezaji wa maziwa kuhakikisha wafugaji wa mkoa wa Njombe hasa wanawake wanakuwa wazalishaji wakubwa wa maziwa na kuhakikisha mkoa wa Njombe unakuwa kinala wa uzalishaji wa maziwa hapa nchini na maziowa ya Njombe kusambaa nchi nzima ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Akizungumza katika maadhinisho ya siku Wanawake ambapo kwa mkoa wa Njombe zimefanyika katika kijiji cha Lole Kata ya Ikuna halmashauri ya Njombe na maandalizi yake kufanywa na wasimamizi wa mradi ukuzaji wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (East Africa Dairy Development, EADD), aliwataka kuhakikisha wanakuza wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa na kuhakikisha maziwa ya Njombe ifikapo mwisho wa mwaka huu yanauza nchi nzima.
Nchimbi alisema kuwa katika ukuzaji wa wafugaji wahakikishe wanawake ndio wanakuwa vinala katika ukuzaji na uzalishaji wa maziwa na kwa kuwa
mkoa wa Njombe kunakuja uwekezaji mkubwa wa uchimbaji wa madini ya
chuma na makaa yam awe wahakikishe wanawezesha mkoa wa Njombe kuwa ndio
unalisha wawekezaji katika machimbo hayo.
“EADD nawataka mhakikishe katika uwekezaji mkubwa unao kuja
hapa nchini na hasa kwa mkoa wa Njombe wawekezaji hawapati maziwa kutoka sehemu
nyingine zaidi ya hapa Njombe na nakata mkoa huu kufunguliwa soko kubwa la
kimataifa la maziwa na liwe ndio la kwanza,” alisema Nchimbi.
Alisema kuwa kufikia mwisho wa mwaka huu mradi huo uwe
umeweza kukuza mwafugaji na maziwa ya kutoka mkoani hapa yanakuwa yamesambaa
nchi nzima na kuwa siko kwamba maziwa kutoka sehemu nyingine yasimame bali
maziwa ya mkoa wa Njombe kwa kuwa yanapenda hivto wahakijishe maziwa haya
yanafika kila kona mikoa ya hapa nchini.
“Kufika mwisho wa mwaka huu nataka kuona kila kona ya nchi
yanafika kwani mimi maziwa ya Njombe nimeanza kuyafahamu kabla sijafuika hapa
Njombe na niliyapenda na maziwa haya yanapendwa na watanzania hivyo wekeni
juhudi ili yafike katika kila kona,” aliongeza Nchimbi.
Naye mkurugenzi mkazi wa mradi EADD, Mack Txsaxo, alisema
kuwa mradi huo unao lenga mikoa ya nyanda za juu kusini ya Mbeya, Iringa na
Njombe kwa tanza nia ni mradia ambao pia upo katika nchi za Uganda, Kenya na
Ruanda umelenga kuinua wafugaji kw akupata kipato kupitia maziwa na marisho.
Alisema kuwa wananchi wa mikoa wa nyanda za juu watapatiwa
uwezeshwaji wa kuboreshewa afya za mifugo yao, kutafutiwa masoko ya uhakika na
kuhakikisha mifigo yao inakuwa yenye manufaa kwao kwa kuboresha ,maisha
kutokana na mazoa ya maziwa.
Aidha mradi huo unatarajia kuwasaidia wafugaji 35,000 hapa
nchini na kufanya wafugaji kuw ana maisha endelevu katika ufugaji wa ngombe wa
maziwa, na kunufaika kimaisha na katika siku ya wanawake mradi huo unatarajiwa
kumsaidia mamamremavu wa macho kwa kumpatia kitu atakacho kiweza katika sekta
ya maziwa.
“EADD itamsaidia mama Anna Ngimbhuchi atasaidia mradi wowote
ambao atakuwa na uwezo nao katika sekta ya maziwa kwa kumpa mtaji wa thamani ya
shiringi milioni moja baada ya wataalam wetu kufanyanae tathimini ya nini
atakiweza kufanya,” alisema Txsoxo.
Aidha baadhi ya wafugaji walio nufakika na kupitia mradhi
huo wameelezea hisia zao na kuwa wamefufaika kuzalisha maziwa mengi zaidi baada
ya kuingia kwa mradi huo na sasa nameweza kuwa na kipato cha kutosha kutokana
na maziwa na uzalishaji wa marisho.
Daina Mangula ni mmoja wa wakazi walio nufaika na mazao ya
Ng’ombe kutokana na maziwa na kuzalisha marisho ambapo akitoa maelezo juu mbele
ya mkuu wa mkoa juu ya faida za malisho alisema kuwa kutokana na mauzi ya mbegu
za marisho bora ya nhombe amefanikiwa kupata kipato cha zaidi ya milioni moja
na kuwa kupitia mauzo ya maziwa ameweza kusomesha watoto na kuwekeza katia
miradi mingine mbalimbali.
Naye afisa mahusiano katika mradi huo Rachael Singo alisema
kwa katika mradi huo wanategemea kuwawezesha zaidi wanawake kwa kuwa wanawake
wakewezeshwa wanaweza kuiinua familia na kuwataka wanawake huhakikisha
wanajiweka katika vikundi ili waweze kufikiwa na mradi huo.