Makarani wapewa onyo uhamiaji haramu

JESHI la Uhamiaji Tanzania, mkoa wa Njombe limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za vitendo vya uhamiaji haramu hasa kipindi hiki cha kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura zoezi ambalo linaendelea mkoani humo.


Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe kamishina msaidizi na kamanda wa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama, alisema kuwa katika zoezi hili linagusa watanzania na kuwa watu wasiowatanza nia hawatakiwi kujiandikisha.


Alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha watu wasio na uraia kuto jiandikisha katika daftari hilo na kuwa kuna askari wanao fuatilia watu ambao sio watanzania kujiandikisha katika daftari hilo la kupigia kura.


“Katika zoezi hili jeshi hili limejipanga na kuhakikisha hakuna mtu anaye jipenyeza kujiandikisha wakati sio raia wa Tanzania, kwa kweli hakuna mtu aliyebainika kujiandikisha ama kutaka kujiandikisha wakati sio mtanzania,” alisema Mhagama.


Kamanda huyo alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo katika halmashauri ya mji mdogo wa Makambako Februari 23 hakuna mtu aliyebainika kutaka kujiandikisha katika daftari hilo linalotarajia kumalizika katika siku ha chache mwishoni mwa wiki.


Aidha alisema kuwa Jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha zoezi hilo halingiliwi na dodari ya kuandikisha watu ambao sio raia wa Tanzania kwa kuwa uraia unatakiwa kupatikana kwa kufuata hatua maalumu.


Alisema kuwa licha ya mkoa wa Njombe kuwa katika mipaka ya nchi ya Malawi na barabara inayo elekea mipaka ya nchi za kusini mwa Afrika jeshi hilo limejipanga kuhakikisha watu watanzania pekee ndio wanaandikishwa na kuwa wamekuwa makini katika uhakikishaji wa kuwa watu wasio watanzania ndio wanaingia nchini.


“Kuhusu hali ya wahamiaji haramu katika mkoa wa Njombe na hasa mipakani tumeendelea kufanya dolia katika maeneo ya pembezoni na mijini hasa wilaya Ludewa ambayo inapakana na nchi ya Malawi na mji wa Makambako amabao unapitiwa na barabara kuu ya kuelekea nchi za kusini mwa Tanzania,” Aliongeza Mhagama


Aliwataka makarani wa uandikishaji wa daftari la kudumu kuwa makini na uchukuaji wa taarifa kwa raia pindi wanapo andikisha kuwabaini watu wasio stahili na kutoa taarifa maramoja sehemu inayo husika kama atabainia mtu ambaye wanamtilia shaka na uraia wake.

Related Posts