SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ,PONGEZI KWA TAWODE.

Kama ilivyo ada leo tarehe nane Machi ni siku ya wanawake Duniani.
N siku ambayo hadhi na heshima ya mwanamke huenziwa bila kujali utaifa, kabila, rangi, dini, utamaduni wake au chama chake cha siasa

Kiasili siku hii haitenganishwi na vuguvugu la wafanyakazi kudai haki na hali bora kufuatia mapinduzi ya viwanda ya karne ya ishirini huko bara Ulaya na Amerika.

Ni vyema ikakumbukwa kuwa sherehe ya kwanza kuenzi siku ya mwanamke ilifanyika mwaka 1909 huko Amerika.

Baadae mwaka 1945 Umoja wa Mataifa ulipitisha makubaliano rasmi ya usawa kati ya mwanamke na mwanamme,kabla ya kuitangaza rasmi tarehe 8 mwezi machi kuwa siku ya wanawake Duniani hii ilikuwa mwaka 1975.

Tanzania, kama nchi nyingine Duniani wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma kimaendelea katika nyanja za elimu na uchumi.

Wakati juhudi kubwa zimefanywa kurekebisha sheria kandamizi kwa wanawake,bado tatizo la kuwapa nguvu wanawake kielimu na kiuchumi ni kubwa hasa kwa jamii za vijijini.

Kwa kubaini tatizo hilo wanawake wa mkoa wa Tanga chini ya Mbunge wao Mh. Ummy Mwalimu (NW) walikaa chini na kuunda taasisi ya kuratibu na kuwasaidia wanawake wa mkoa mzima wa Tanga. Taasisi hii hujulikana kama TAWODE yaani Tanga Woman Development, ikiwa na makao yake makuu Tanga  mjini.

Kushoto ni mfanyakazi wa TAWODE, Kulia ni msichana aliyefaidika na mpango wa TAWODE.

Wanawake wa Tanga wakipata elimu ya ujasiriamali toka TAWODE.
Wanawake Tanga wakiwa pamoja na mwenyekiti wa TAWODE.
Kwa muda mfupi wa miaka miwili TAWODE imefanikiwa kutoa elimu ya ujasirimali na afya kwa wanawake katika wilaya zote za mkoa wa Tanga.Pia imefanikiwa kutengeneza mpango unaowasaidia watoto hasa wa kike kupata mahitaji muhimu wakiwa shule ikiwa ni pamoja na ada.

Tafiti zinaonesha kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kusomesha kaya nzima, HONGERENI TAWODE HONGERANI WANAWAKE WOTE

Related Posts