KWA siku nzima ya leo wafanyabiashara wamefunga maduka yao kwa kilekinacho daiwa kuwa ni kuwa katika siku ya kesi ya mwenyekiti wao wa taifa wa jumuia ya wafanyabiashara JWT, Taifa John Minja.
WAFANYABIASHARA mkoani Njombe na mji mdogo wa Makambako
walifunga maduka kwa zaidi ya masaa 6 Siku ya juzi na kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya mfanyabiashara mwenzao ambaye alipandisha mahakamani kwa mara ya kwanza Februari 6 mwaka huu na
baadae kufanya mkutano wao.
Mfanyabiashara mwenzao Maxson Sanga alipandishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi Njombe Februari 6 mwaka huu na mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) kwa kile lilichodaiwa kuwazuia kuwazuia kufanya kazi zake na kudai
kuivunja sheria ya kodi namba 4 ya mwaka 2004.
Sanga alipandishwa mahakamani na wasimamizi wake wawili wa
kampuni yake ya Mexons Investment Co. Ltd akiwemo Meneja wa Kampuni hiyo Emma
Mgeni, na mkewe Happy kwa mashtaka ya kudaiwa kuwagomea maofisa wa mamlaka ya
kukusanya mapato kanda ya Mbeya (TRA) waliofika katika eneo lake la biashara
kwa lengo la kumkagua biashara yake.
Kesi hiyo iliyo wafanyawafanyabiashara kufunga maduka yao na
kusababisha wakazi wa Mjini Njombe na baadhi ya wafanyabiashara kutoka
makambako iliahilishwa kwa kuwa wakili upande wa TRA kuwa nje ya mji na
kuifanya hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi wa mahakama ya Njombe,
Augustine Rwinzile kuiahilisha mpaka Aprili 8.
Katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe polisi wa kutuliza
ghasia (FFU) wakiwa na gari moja la polisi lenye namba za usajili PT 1864 na
zaidi ya askari wasiopungua 18, walikuwepo mahakamani hapo kwa lengo la kuangalia usalama huku
wakiwa wamejiandaa kwa mabomu ya machozi huku wakiwa wamevalia mavazi ya
kupambana na vurugu.
Baada ya kesi hiyo kuahilishwa kwa kesi hiyo wafanyabiashara
wote waliondoka kwa umoja wao kuelekea katika ukumbi wa mikutano wa Turbo huku
wakifiatiliwa nyuma na polisi hao na mkutano wao kulindwa na askali hao mwanzo
mpaka mwisho kukiwa kumetawala amani ya kutosha katika ukumbi huo na wafanyabiashara waliokuwa nje ya ukumbi
kuambiwa waingie ndani na kupewa onyo na askali aliyekuwa amevaa mavazi ya
kuraia.
Mkutano huo uliodumu kwa masaa zaidi ya manne ulifunguliwa
na mwenyekiti wa korido ya wafanyabiashara wakubwa na wenye viwanda (TCCIA)
mkoa wa Njombe Oraph Mhema ambaye aliwataka wafanyabiashara hao kuwa na umoja
katika biashara zao na kupinga matendo mbalimbali ya rushwa na yanayo shawishi
rushwa yanayo fanywa na TRA.
Alisema kuwa moja ya mambo ambayo wafanyabiashara wanatakiwa
kuweka wazi ni pamoja na TRA kutumia madalali kukusanya kodi wakati wao
wanalipwa mshahara kwaajili ya kukusanya kodi za watanzania.
“Wafanyabiashara ntatakiwa kuweka wazi na kutoa taarifa
mapema mnapoona kuna dalili za kufanyiwa vitendo vya kuwashawishi kutoa rushwa,
TRA wamekuwa wakiwatumia madalali kukusanya kodi na makufuli yao kufunga maduka
yenu yakiwa na nembo za TRA, kitu hicho tunatakiwa kukipiga vita kwa sababu
maofisa wanalipwa kwaajili ya kazi ya kukusanya kodi haiwezekani tukalipa kodi,
madalali na maofisa,” alisema Mhema.
Aliongeza kuwa: "Kama hatutaungana wafanyabiashara kwa
dhati, hakika hatutasonga mbele, meneja wa TRA mkoani Njombe tulizungumza nae
kuhusu kesi inayomkabili mwenzetu Mexons alisema hana kosa, maofisa wa TRA
walifanya oparesheni bila yeye kupata taarifa," alisema Mhema.
Mhema alisema kuwa hata hivyo kufuatia kesi inayomkabili
mfanyabiashara huyo, Mexons ameombwa atoe shilingi laki mbili ili kesi hiyo
ifutwe, jambo ambalo Mhema alisema wamepinga kutolewa fedha hizo na badala yake
kumtaka aliyeifungua kesi hiyo ndiyo wanaopaswa kulipa fedha hizo.
Aidha katika hatua nyingine, Mhema alisema Kamishna Mkuu wa
TRA nchini atakutana na wafanyabiashara wote mjini Makambako Machi 7 mwaka huu
katika ukumbi wa Green City uliopo mjini Makambako kwa ajili ya kuzungumzia
kupinga ongezeko la kodi la asilimia 100.
Naye Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara mjini
Makambako, Siphaely Msigala alisema katika kikao kitakachofanyika Machi 7 na
Kamishana Mkuu wa TRA mjini Makambako, wafanyabiashara wote wametakiwa kufunga
biashara zao kwa ajili ya kwenda kuzungumza na Kamishna huyo.
Alisema kuwa katika mkutano huo kutakuwa na Mkuu wa Mkoa Dk.
Rehema Nchimbi, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, Wakurugenzi wa
Halmashauri ya mji wa Makambako na Halmashauri ya Mji Njombe pamoja na kamanda
wa polisi, Fulgence Ngonyani .
Alisema lenho la kuwaalika viongozi hao wa juu ni kuja kujua
matatizo yao wakati wanawasilisha kwa kamishina wa TRA taifa.