MAAFISA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MAFAO YA UZEENI KENYA (RBA) WAFURAHISHWA NA HUDUMA ZA PPF




Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate, (kulia), na Meneja Miundombinu ya IT wa Mfuko huo, Gilbert W. Chawe, (katikati), wakimsikiliza afisa mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Rehema Kabongo, wakati wa ziara ya Maafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mafao ya Uzeeni, nchini Kenya, (RBA), kwenye makao makuu ya PPF barabara ya Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam.
Maafisa toka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tanzania, (SSRA) na wenzao kutoka Kenya (RBA), wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na mameneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati maafisa hao walipotembelea makao makuu ya PPF kwa nia ya kujifunza shughuli za uhifadhi wa mafao na pensheni.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifuatilia kwa makini wakati wa mkutano baina ya viongozi wa PPF na maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao Ya Uzeeni kutoka Kenya, (RBA), walioongozwa na wenyeji wao SSRA kwenye ziara yao ya kujifunza walioifanya makao makuu ya Mfuko huo barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam.
Afisa mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao ya Uzeeni nchini Kenya, (RBA), Timoth Chege, (kushoto), akiuliza swali wakati wa mazungumzo baina ya maafisa hao kutoka Kenya walioongozwa na maafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, nchini SSRA na uongozi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa ziara ya maafisa hao kwenye makao makuu ya PPF jijini Dar es Salaam, Kulia ni Rehema Kabongo kutoka SSRA.
Meneja wa Huduma kwa Wanachama, wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Godfrey Mollel, (wanne kushoto), akitoa maelezo kwa maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao ya Uzeeni nchini Kenya, (RBA), na wale wa SSRA, wakiangalia jinsi mfumo wa kuhudumia malipo kwa wastaafu unavyofanya kazi wakati walipotembelea makao makuu ya PPF jijini Dar es Salaam kwa nia ya kujifunza.
Meneja wa Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Godfrey Mollel, (wa pili kushoto), akitoa maelezo jinsi idara yake inavyohudumia wateja kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya kupitia njia ya simu, wakati wa ziara ya Maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mafao wa Wastaafu nchini Kenya (RBA), wealiofuatana na wenyeji wao wa Tanzania SSRA, wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Vupe Ligate, na wa kwanza kushoto ni afisa kutoka SSRA Rehema Kabongo.
Meneja wa Miundombinu ya IT wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gilbert W Chawe, (kulia), akitoa maelezo wakati ujumbe huo wa RBA kutoka Kenya, ulipotembelea chumba cha wataalamu wa compyuta wa PPF.