WAALIMU nchini wametakiwa kuanza kununua hisa katika benki yao inayo tarajiwa kufunguliwa hivi karibuni na kuwa itaanza benki kubwa hapa nchini tofafauti na benki zingine zinazo funguliwa.
Akizungumza wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama cha waalimu wilaya ya Wangingombe Mkoani Njombe, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kuuza hisa jijini Dar es Salaam (ZanSecurities) Raphael Masumbuko alisem akuwa waalimu wachangamkie fursa la kununua hisa katika benki yao.
Alisema kuwa zoezi la ununuzi wa hisa katika benki yao ambazo zitaisogeza katika hatua za kufunguliwa kwake ambapo watanunua hisa zao kwa shilingi 500.
Alisema kuwa benki ya Waalimu Tanzania na kuwa pesa imetengwa kwaajili ya kuifungua bengi hisyo kiasi cha shilingi Bilioni 15 kwaaji li ya kufungulia benki hiyo huku kukisubiliwa kununuliwa kwa hisa ambapo wanao lengwa katika hisa hizo ni waalimu na watanzania kwa ujumla.
Masumbuko alisema kuwa benki hiyo inatarajiwa kufunguliwa kwa shilingi bilioni 25 na kuwa hisa zitauzwa za zaidi ya shilingi bilioni 10 ili kufikia lengo la kufungua bengi hiyo.
Alisema kuwa zoezi la uuzwaji wa hisa litaanza machi 23 na kuwa waalimu watatakiwa kufika katika benki ambazo ni wakala wa soko la hisa na kupata kwa kununua kupitia simu zao za mkononi kwa kupiga *150*136# ambapo waalimu watapata fulsa za kununua hisa za benki yao ya waalimu Tanzania huku zoezi hili likitarajiwa kusitishwa Mei 4 mwaka huu.
Alisema kuwa baada ya kuuzwa kwa shilingi 500 mwa mda huo huenda hisa hizo zitapanda bei na kuuzwa zaidi ya shilingo 500 na huku kila mwalimu akitakiwa kununua hisa zisizo pungua 100 kama za kuanzia.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa chama cha waalimu mkoa wa Njombe, Ally Mbaga, aliwataka waalimu kuhakikisha wahapitwi na fulsa lya kununua hisa kwaajili ya manufaa yao ya baadae ambapo watapata fulsa ya kupata kawio baada ya benki kupata faida.
Aliwatoa waalimu wasiwasi wa kutapeliwa kuhusiana na mfumo wa kununua hisa hizo ambapo mfumo hua ameutaja ni kama ule unaotumika katika usafirishaji wa fedha kwa njia ya mtandao katika simu ambao tumeingia hivi karibu na waondokane na wasiwasi wa matapeli wa kimtandao.
“Waalimu mukakikishe mnanunua kwa wingi hisa katika benki yenu ili hapo baadae munufaike na magawio kutoka benki yetu mkizubaa watu wengine watanunua hisa wakati ninyi mpo, na haipendezi kuangalia maslahi mapema kabla ya kuwekeza kununua hisa unawekeza,” alisema Mbaga
Aidha katika uchaguzi huo waalimu wilaya ya Wangingombe walipata uongozi mpya ambao utasukuma kijiti cha uongozi kwa Chama cha Waalimu wilaya hiyo kwa miaka mitano huku wakimpata mwenyekiti.
Akisoma matokeo katika uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni katibu wa mkoa Mbaga alimtaja Andrew Twamalika kuwa mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Wangingombe.
Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti Twamalika alisema kuwa waalimu wanatakiwa kuonyesha ushirikiano katika kipindishake hichi cha uongozi na kuahidi kuhakikisha mipango iliyo anzishwa na wenzake kukamilika na kufungua miradi mingine mbalimbali.