MKUU wa wilaya ya Wangingombe Asumpta Mshama amaesema kuwa
tatizo la ufauulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 Kushuka linatokana na
uzembe wa walimu na sio wazazi wala wanafunzi linatokana na uzembe walimu kujihusisha
kimapenzi na wanafuzi pamoja na tabia ya baadhi yao kujihusisha na mambo ya
kisiasa
Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha walimu wakuu
wa shule za sekondari wilayani humo pamoja na wakuu wa bodi amesema kuwa shule
nyingi wilayani humo zinamazingira mazuri ya kufaurisha yenye madarasa mazuri
mabweni na maabara jambo ambalo alisema linaonyesha kuwa wazazi wamehamasika
kuchangia elimu lakini walimu ndio kikwazo
Mkuu huyo wa wilaya alitumia kikao hicho kuwaagiza wakuu wa
shule kuhakikisha wanawasimamia walimu kufundisha na kujiepusha na vitendo
visivyofaa hasa mapenzi shuleni huku akiwaagiza
kushirikiana na watendaji kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wazazi ambao
hawajawapeleka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza
Miongoni mwa sababu za
ufaulu kushuka katika shule za sekondari wilayani humo imetajwa kuwa ni
pamoja na walimu na wanafunzi kukosa chakula cha mchana, Mwingiliano wa elimu
na siasa huku wengine wakisema walimu wanajihusisha na shuguli za ujasiriamali
na kilimo kama bodaboda anaeleza Henry
nyimbo mwenyekiti wa bodi shule ya sekondari luduga na mwalimu mkuu wa
sekondari ya ilembula Vituce Mpogole
Wakitoa taarifa za wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha
kwanza mwaka 2016 baadhi ya walimu wakuu akiwemo Optatus mng'ong'o mkuu wa
shule ya sekondari ya wanging'ombe wamesema baadhi ya wanafunzi wametoroka
pamoja na wazazi wao huku wengine wakiwa ni yatima pamoja na kueleza changamoto
za mapokeo ya wazazi juu ya dhana ya elimu bure
inaathiri maendeleo ya elimu
Hata hivyo mkurugenzi wa wilaya hiyo Merkzedeki Humbe amesema
walimu waliowengi wanapenda kukumbilia kujiendeleza Kimasomo na kuacha shule
zikiwa na mapengo ya walimu na hivyo amegiza walimu wakuu kuhakikisha
wanaruhusu walimu kwa kuzingatia uhitaji wa shule huku akieleza kuwa sifa ya
mwalimu kupata nafasi ya kujiendeleza iwe ni kufaulisha kwa kiasi kikubwa
Wilaya wanging'ombe ina shule za sekondari 17 na ufaulu wa
mwaka 2014 ulikuwa ni asilimia 77 huku ufaulu wa mwaka 2015 ukishuka na kufikia
asilimia 72 na idadi kubwa ya wanafunzi wamefeli kwa kupata madaraja ya dision 0 na 4