Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

FAIDA 10 YA JUISI YA UKWAJU


Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU. 

  • Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets
  • Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu   baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni  uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu 
  • Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe  andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe 
  • Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.


FAIDA YA JUISI YA UKWAJU. 

  • Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  • Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  • Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  • Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  • Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  • Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  • Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  • Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  • Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  • Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!
Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla

Watu waishio bara la Asia, Carribian na America ya kusini,wanajua kuwa kula ukwaju maana yake ni Afya Njema.

Ukwaju unaoliwaa katika maeneo haya maeneo hayo una faida nyingi kwa watu wanaoula.
Kwa hiyo siku nyingine unapoenda kufanya manunuzi ya vyakula hakikisha unanunua na ukwaju.
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia ambalo limefungwa na kasha gumu. Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani yake kuna mbegu nyeusi. Vifundo hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na faida za kiafya za ukwaju. 

Ukwaju una ladha faluni ya uchachu ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu kadiri unavyokuwa na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.

Katika nchi kama Jamaica, Mexico, Aruba na India, ukwaju unachanganjwa na sukari na kuuzwa kama pipi katika mitaa na madukani. Kula ukwajua au bidhaa zitokanazo na ukwaju kuna faida sana. Ukwaju umejaa Vitamini, fiber, potassium, magnesium na virutubisho vingine muhimu kwa afya njema.

Lakini kati ya faida zingine nyingi za virutubisho na kiafya za ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni za muhimu zaidi, na ni kama zifuatazo:

  1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha antioxidants ambazo zinasaidia kupigana na saratani. Ukwaju una carotenes, Vitamini C, flavanoids na vitamin B zote.
  2. Ukwaju unakuepeusha na ukosefu wa Vitamini C.
  3. Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya mafua.
  4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni.
  5. Ukwaju unakusaidia kutibu matatizo ya nyongo.
  6. Juisi ya ukwaju hutumika kama kitu cha kustarehesha mwili.
  7. Ukwaju unapunguza cholesterol mwilini.
  8. Ukwaju unasaidia kuwa na moyo wenye afya njema.
  9. Ukwaju ukiunywa unasaidia kupooza koo.
  10. Ukwaju ukiupaka kwenye ngozi unasaidia kutibu uvimbe Kwa Tanzania ukwaju unapatikana kwenye masoko karibu yote. 
    Ninakushauri kutengeneza juisi ya ukwaju nyumbani kwako na weka sukari kidogo na juisi hiyo iwe sehemu ya chakula chako. Kama wewe unapenda kula hotelini au kwenye vioski basi agizo juisi ya ukwaju ikusaidi kushushia chakula
    Mapenzi na siasa vyadaiwa kushusha ufauru

    Mapenzi na siasa vyadaiwa kushusha ufauru

    MKUU wa wilaya ya Wangingombe Asumpta Mshama amaesema kuwa tatizo la ufauulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 Kushuka linatokana na uzembe wa walimu na sio wazazi wala wanafunzi linatokana na uzembe walimu kujihusisha kimapenzi na wanafuzi pamoja na tabia ya baadhi yao kujihusisha na mambo ya kisiasa

    Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha walimu wakuu wa shule za sekondari wilayani humo pamoja na wakuu wa bodi amesema kuwa shule nyingi wilayani humo zinamazingira mazuri ya kufaurisha yenye madarasa mazuri mabweni na maabara jambo ambalo alisema linaonyesha kuwa wazazi wamehamasika kuchangia elimu lakini walimu ndio kikwazo

    Mkuu huyo wa wilaya alitumia kikao hicho kuwaagiza wakuu wa shule kuhakikisha wanawasimamia walimu kufundisha na kujiepusha na vitendo visivyofaa hasa mapenzi shuleni huku akiwaagiza  kushirikiana na watendaji kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wazazi ambao hawajawapeleka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza
     
    Miongoni mwa sababu za  ufaulu kushuka katika shule za sekondari wilayani humo imetajwa kuwa ni pamoja na walimu na wanafunzi kukosa chakula cha mchana, Mwingiliano wa elimu na siasa huku wengine wakisema walimu wanajihusisha na shuguli za ujasiriamali na kilimo kama bodaboda  anaeleza Henry nyimbo mwenyekiti wa bodi shule ya sekondari luduga na mwalimu mkuu wa sekondari ya ilembula Vituce Mpogole

    Wakitoa taarifa za wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2016 baadhi ya walimu wakuu akiwemo Optatus mng'ong'o mkuu wa shule ya sekondari ya wanging'ombe wamesema baadhi ya wanafunzi wametoroka pamoja na wazazi wao huku wengine wakiwa ni yatima pamoja na kueleza changamoto za mapokeo ya wazazi juu ya dhana ya elimu bure  inaathiri maendeleo ya elimu

    Hata hivyo mkurugenzi wa wilaya hiyo Merkzedeki Humbe amesema walimu waliowengi wanapenda kukumbilia kujiendeleza Kimasomo na kuacha shule zikiwa na mapengo ya walimu na hivyo amegiza walimu wakuu kuhakikisha wanaruhusu walimu kwa kuzingatia uhitaji wa shule huku akieleza kuwa sifa ya mwalimu kupata nafasi ya kujiendeleza iwe ni kufaulisha kwa kiasi kikubwa

    Wilaya wanging'ombe ina shule za sekondari 17 na ufaulu wa mwaka 2014 ulikuwa ni asilimia 77 huku ufaulu wa mwaka 2015 ukishuka na kufikia asilimia 72 na idadi kubwa ya wanafunzi wamefeli  kwa kupata madaraja ya dision 0 na 4

    Kategori

    Kategori