DAFTARI CHANGAMOTO KIBAO


DAFTARI la kudumu la mpiga kura katika halmashauri ya Makete nako limeghubigwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya printa kutofanyakazi vizuri katika siku ya kwanza na kuandikisha watu 2153 huku mtu mmoja vitole kushindwa kabisa kusoma na kurudishwa nyumbani.

Akizungumza na ELIMTAA MEDIA Wilayani Makete jana, kaimu afisa uchaguzi wa wilaya ya Makete Gregory Emmanuel,  alisem akuwa zoezi hilo linaenda vizuri katika halmashauli hiyo licha ya kuwepo changamoto mbalimbali za mashine.

Alisema kuwa kwa siku ya kwanza Machi 16 walifanikiwa kuwaandikisha watu 2153 katika vituo walivyo vitenga kulingana na mashine walizo napewa na tume, 38 na zinazo fanya kazi ni mashine 36 huku mashene mbili zikibaki za ziada kwaajili ya dharula.

Emmanuel alisema kuwa halmashauri yake kuna vituo 36 ambavyo vimechukua kata 5 za na siku ya pili walifanikiwa kuandikishwa 2479 na kuwa idadi ya watu imeongezeka kutokana na uzoefu unavyo ongezeka wa watu wanao andikisha.

“Katika halmashauri hi watu wameongezeka siku ya piki walioandikishwa ni kutokana na spidi ya wanao andikisha kuongeza kasi na changamoto siku ya pili hazi kuwepo nyingi kama siku ya kwanza na siku ya kwanza mashine zilikuwa sinasumbua hasa printa zilikuwa zinaprinti picha nyeusi au nyeupe lakini mafundi walijitahidi kurekepbisha,” alisema Emmanuel.

Alisema kuwa mbali ya changamoto za mashine kuharibika pia wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kimazingira ambapo kunamazingira mvua zikinyesha barabara hazipitiki hivyo kunamaeneo mashine zimechelewa kufika kutokana na tatizo hilo la miundombini ya barabara.

Alisema kuwa katika halmashauri yake siku ya pili ameshuhudia mtu mmoja ambaye alishindwa kuandikishwa kutokana na usugu wa mikono yake na mashine kushindwa kuchukua alama za vidole vyake.

Alisema mtu huyo alitakiwa kurudi nyumbani kutokana na kushindwa kuchukuliwa alama zake za vidole na hajajua hatima ya mwananchi huyo kwa kuwa hajawasiliana na ye kama amerudi.

“Kutokana na wananchi wa halmashauri hii kuwa na kazi ngumu za mikono mwananchi mmoja niemshuhudia akirudishwa nyumbani baada ya kutochukuliwa kwa alama za mikono yake na alijaribu zaidi ya mara saba, na kutumia mda mrefu hadi dakika 30 wakati wakifanya juhudi za kuirazimisha mashine isome,” alisema Emmanuel.

ELIMTAA MEDIA imeshuhudia watu wakiwa wamehamashina na kuwa wavumilivu katika mistali ya kusubiri kuandikishwa na watu wakitumia dakika zaidi ya 15 hadi anapo toka na kitambulisho.

Baadhi ya wananchi wamesema kuwa wamekuwa wakiwahi katika vituo vya kujiandikisha wengi wao wakisema wanawahi foleni majira ya saa 11 alfajili na kukuta wenzao wakiwepo katika foleni na kufikia majira ya saa tano ndipo kujikuta wakiandikishwa.

John Sanga ni mmoja wa wakazi ambao waliwahi majira ya saa 11:00 alfajiri na kujikuta inafika saa 5:00 asubuhi kupata kitamulisho chake.

Baadhi yao wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya vitambulisho hivyo huku wengi wao wakijiandikishwa kwaajili ya kupigia kura pekee na wengine wakitaka kwaajili ya kutamulika.