CCM wawekewa pingamizi Njombe


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Njombe kimemuwekea pingamizi mgombea wa Chama cha Mapindusi CCM, kiti cha Ubunge jimbo la Njombe Kusini Edward Mwalongo, na kusema kuwa hawana imani na msimamizi wa uchaguzi msaidizi wa jimbo hilo.

Akizungumza na Elimtaa blog Mkoani Njombe jana Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe Ally Mhagama alisema kuwa Chadema wamemuwekea pingamizi mgombea wa CCM ambaye katika fomu yake inadaiwa kuwa alijaza kuwa aliwahi kuhukumiwa kwa makosa ya jina kitu kinacho mnyima sifa ya kuwa mgombea.

Mhagama alisema kuwa mgombea huyo sehemu ya kujaza kama aliwahi kuhukumiwa au hajawahi kuhukumiwa alijaza kuwa aliwahi huhukumiwa na kuapa mbele ya mahakama kuwa alichokijaza katika fomu hizo kuwa ni kweli.

Mgombea wa Chadema kiti cha Ubunge, Emmanuel Masonga alisema kuwa licha ya kuona kuwa mgombea wa CCM alijaza kuwa aliwahi kuhukumiwa lakini msimamizi wa uchaguzi msaidizi wa jimbo hilo ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Njombe alimrekebishia fomu hiyo siku ya jumamosi majira ya saa 7 arasili na kuwa kitu ambacho ni kinyume na taratibu ambazo fomu ilitakiwa kujazwa na kukabidhiwa kwa tume siku ya Ijumaa saa kumi.

Alisema kuwa Chama hicho hakina imani na msimamizi wa uchaguzi kwa kuwa amefanya marekebisho ya fomu ya mgombea kwa kuwa anaweza kufanya mambo yasiyo faa katika uchakuzi na kuwa hawako tayari kupokea maelekezo kutoka kwa msimamizi hiyo.

Alisema; “Mgombea katika sehemu ya kuwa aliwahi kushitakiwa ama laa alijaza kuwa aliwahi kushitakiwa na baada ya kupeleka pingamizi jana (Jumamosi) majira ya saa saba mchana msimamizi alibadilisha katika fomu hiyo lakini katika mabadiliko hayo bado kuna shida ya kuwa hawajakata sehemu ya kukubari na kukataa kuwa aliwahi kushitakiwa ama laa bado licha ya kuandika hapana lakini hawajakata kuwa hakuwahi kushitakiwa,” alisema.

Alisema kuwa siku ya jumapili wamepeleka mapinga mizi tume ya uchaguzi makao makuu na kuwa katika ngazi ya jimbo wamepeleka nakala.

Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi wa jimbo lala Njombe kusini Venance Msungu alisema kuwa siku ya jumamosi walipokea pingamizi kutoka Chadema dhidi ya mgombea wa CCM ambapo waliwasilisha pingamizi alirekebisha makosa katika fomu hiyo.

Alisema kuwa kosa la mgombea huyo lilikuwa ni la kimakosa ya kawaida na kuwa kama wana uhakika na walicho kijaza basi walete udhibitisho wa kimahakama ambao unaeleza kuwa aliwahi kishitakiwa na kuwa watayapokea na kufanyia kazi.

Alisema kuwa pingamizi lao halina ushahidi na kuwa watapokea kama zitakuja hukumu za wahusika.

Upande wa katibu wa CCM wilaya ya Njombe, Saadi Kimati, amesema kuwa katika ujazaji wa fomu kipengele hicho kilijazwa kimakosa na kuwa ndio maana sehemu ya kutoa maelekezo palibaki bila kutoa maelezo.


Alipo ulizwa ngombea wa CCM Edward Mwalongo ambaye amewekewa pingamizi na Chadema alisema kuwa hajapokea taarifa zozote kuhusiana na kuwapo kwa pingamizi hili na anatarajia kama lipo kupokea kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi.

Kwa upande wa tume ya uchaguzi (Nec) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva amesema kuwa kwa malalamiko ya majimbo yatafika kwao kama hayatashugulikiwa kutoka katika jimbo husika.

Hivyo kwa pingamizi lililowekwa na Chadema kwa jimbo la Njombe bado halijafika katika ofisi ya Tume taifa na kuwa Mkurugenzi anaweza kurekebisha makosa madogo madogo ya kiuandishi.