WAKURUGENZI watendaji wa halmashauri za mikoa ya Njombe na Ruvuma wameiomba serikali kuwawekea ulinzi wa kutosha wakati wa uchaguzi ili kulinda maisha yao baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa kuwa matokeo yatakayo tolewa hayata furahisha baadhi ya upande.
Hayo yamebainishwa katika semina ya siku mbili ya kuwakumbusha wakurugenzi na wasimamizi wa uchaguzi kwa ngazi ya wilaya wa halmashauri za mikoa ya Ruvuma na Njombe kwa kanda ya nyanda za juu Kusini yaliyo endeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nec mwishoni kwa wiki hii.
Wakurugenzi hao wameomba ulinzi wakati wa kuanza uchaguzi, na baada ya kutangaza matokeo kwa muda ili kuwaweka salama kwa kuwa matokeo ya uchaguzi yanakuwa yameumiza upande fulani kwa kuwa kuna usindi na upande utashindwa.
Akiuliza shwali kwa Tume ya uchaguzi taifa Nec Mkurugenzi wa halamashauri ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Ally Mpenye, alisema kuwa wamekuwa na wasiwasi wakati wa kutangaza matokeo hivyo Tume na serikali kwa ujumla ihakikishe kuwa watumishi na wahusika wa utangazaji wa matokeo wahakikishiwe ulinzi wa kutosha wakati wote wa uchaguzi ili kuyaweka maisha yao salama.
Aliongeza kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na ulinzi lakini haukuwa wa muda mrefu na kuongeza kuwa ulinzi huo uanzie kazini mpaka nyumbani.
Aidha mkurugenzi wa halmashauri ya Wanging'ombe Melkizedeck Humbe aliiomba Tume kuhakikisha kuwa vifaa vya uchaguzi kusambazwa mapema kutokana na baadhi ya halmashauri kuto fikika vizuri na huenda kukasababisha kutofika kwa wakati kwa vifaa mihimu na kuwa ihakiki vifaa hivyo mapemba ili kutotokea usumbufu wa vifaa ambavyo havija kamilika.
Humbe alisema kuwa kama tume imesema kuwa vifaa vitafika Octoba 24 ni bora vika wahi kidogo ili kudhibitu ukosefu wa vifaa wakati muda umefika kwa kuwa baadhi ya maeneo hayafikiki kwa urahisi.
Aidha tume ilisema kuwa vifaa na elimu kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao vinaenda kwa vipindi na kuwa vifaa vitapelekwa katika vituo Octoba 24 na kuwa ndivyo ratiba yao inavyo sema.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa wa uchaguzi Kanda ya nyanda za juu Kusini Jane Tungu alisema kuwa tume ratiba yake inasema kuwa kuna vifaa vina wahi katika vituo lakini kama karatasi za kupigia kura hazina haja ya kuwahi kufika katika vituo ndio maana zinapelekwa siku moja kabla ya kupiga kura.
Kwa upande wake mgeni rasimi aliyefungua semina hiyo Katibu tawara wa mkoa wa Njombe Jacson Saitabahu kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Rehema Nchimbi alisema wasimamizo wakakikishe kuwa hawafanyi kazi kwa mazoea bali wafanye kazi hiyo kwa uzoefu wa kuelewa kanuni za uchaguzi.
Alisema kuwa Uchaguzi ukikosema hakuna samahani na utaenda na mtu kwa kufukuza hakutakuwa na msalia mtume kwa hiro na kuwataka kuwa makini wakati wa kusimamia uchaguzi kwani ni sehemu ya mihimu katika nchi.
Katibu tawara wa mkoa wa Njombe Jacson Saitabahu |