Mtoto wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Salmin Amour, Amini Salimini Akanusha Uvumi ulioko katika Mitandaoo ya Kijamii


Afisa Habari Muandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ndg Ramadhani Ali, akiongoza mkutano wa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati wa mkutano wa kukanusha taarifa znazosambazwa na baadhi ya Watu katika mitandao ya Kijamii kuhusiana na Mtoto wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Amini Salimini kuhama Chama na kujiunga na Chama cha Upinzani.   
Aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Mkwajuni Mtoto wa Rais Mastaaf wa Zanzibar Dk Salmin Amour Juma, Amini Salmini Amour akikanusha habari zinazosambazwa na baadhi ya Watu kuwa anataka kuhama Chama cha Mapinduzi na kujiunga na Chama cha Upinzani, Amekanusha habari hizo kuwa sio za kweli na yeye bado Mwana CCM na ataendelea kuwa Mwanachama Mtii wa Chama cha Mapinduzi. 
Amesema habari hizo si za kweli ni uzushi na kutaka kumuharibia jina lake na la Baba yake na kusisitiza yeye atabakia kuwa CCM. 
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.

Amini Salmin Amour akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma hizo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.