Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed
Shein akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha
na biashara ya Kuuza Kuku (Perdue)kutoka Marekani Dk.David Elua
akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja jana kwa
mazungumzo
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
1.10.2014
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa hatua ya Kampuni ya ZANCHICKS
kuekeza Zanzibar zitaweza kufikisha malengo ya uekezaji hapa nchini sambamba na kuinua soko la ajira na kukuza
uchumi.
Dk. Shein
aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya
ZANCHICK huko Ikulu mjini Zanzibar. Kampuni ambayo kwa hivi sasa
inajishughulisha na uagizaji wa malighafi zake kutoka nje ambazo ni nyama ya
kuku na kuuza hapa nchini.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Katika maelezo
yake Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa miongoni mwa azma na malengo la
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuinua sekta ya uekezaji ni kuhakikisha
wananchi wake wanapata ajira hatua ambayo pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa
nchi.
Dk. Shein alisema
kuwa kuanzisha biashara ya nyama ya kuku hapa nchini kunatoa fursa kwa wananchi
kutumia chakula hicho ambacho kimekuwa na walaji wengi hivi sasa sambamba na
kuimarika kwa wafanyabiashara hiyo hapa Zanzibar.
Aidha, Dk. Shein
aliueleza uongozi huo haja ya kutoa ushirikiano na msaada mkubwa kwa
wafanyabiashara wa aina hiyo wazalendo hapa Zanzibar ambao nao pia, wanahitaji
kuimarika zaidi kibiashara kama ilivyo kwa kampuni hiyo hivi sasa.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Dk. Shein
alisisitiza kuwa hatua hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara
wazalendo kuweza kuimarika kibiashara hali ambayo itasaidia lengo la Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar katika kupambana na umasikini pamoja na kufikia lengo la
Dira 2020 katika ukuaji uchumi wa Zanzibar.
Pamoja na hayo,
Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia
Wizara pamoja na Taasisi zake husika zitaendelea kutoa ushirikiano wake kwa
Kampuni hiyo ili kuhakikisha inaendelea kufanya shughuli zake kwa ufanisi
zaidi.
Dk. Shein
aliueleza uongozi huo kuwa soko la biashara hiyo kwa hapa nchini ni kubwa sana
hivyo, jambo kubwa linalohitajika ni kuendeleza na kupanua soko la biashara
hiyo ili Kampuni hiyo iweze kupata mafanikio zaidi na kufikia lengo
ililojiwekea katika biashara zake.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Sambamba na hayo,
Dk. Shein aliueleza uongozi huo kuwa katika biashara yoyote ile suala la
ushindani wa kibiashara haliepukiki hivyo, ni jambo la busara kwa Kampuni hiyo
kufanya biashara zake kwa kuwavutia watumiaji pamoja na kutoa ushirikiano kwa
jamii.
Nae kiongozi wa
Kampuni hiyo Dk. David Elua alimueleza Dk. Shein kuwa Kampuni yake imeweza
kupata mashirikiano mazuri kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara
husika na Taasisi zake zote na kupongeza kwa hatua hiyo ambayo imeiwezesha
Kampuni ya ZANCHICK kufanya shughuli zake kwa ufanisi mkubwa hapa Zanzibar.
Dk. Elua alieleza
kuwa Kampuni yake kwa hivi sasa tayari imeshatoa ajira kwa vijana zaidi ya 300
wa hapa Zanzibar wakiwemo wanaofanya kazi kiwandani pamoja na wasambazaji wa
bidhaa zake.
Ads by 1ClickMovie-Download1.1Ad Options
Aidha, kiongozi
huyo, alimueleza Dk. Shein azma ya Kampuni ya ZANCHICKS ambayo imeanza shughuli
zake hapa nchini mnamo mwaka 2011, kuanzisha Kiwanda cha kusarifu bidhaa za
kuku na kusafirisha nje ya nchi sambamba na kupanua zaidi soko la ajira kwa
wananchi wa Zanzibar.
Kiongozi huyo wa
Kampuni ya ZANCHIKS yenye Makao Makuu yake nchini Marekani alieleza kuwa
Kampuni hiyo inafanya biashara zake katika maeneo mbali mbali duniani pia,
alieleza kuwa taratibu za utayarishaji
wa kuku hao ni halali.
Sambamba na hayo,
Dk. Elua alieleza mafanikio yaliopo katika shughuli za Kampuni hiyo hapa
Zanzibar na kueleza azma ya Kampuni yake kupanua zaidi soko la nje ya nchi
licha ya baadhi ya changamoto zilizopo.