Wagombea Uwakilishi na Udiwani wa Chama cha ADC.


Afisa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Ndg. Mohammed Ali Abdallah akiwasomea wagombea baadhi ya vipengele vya fomu za kugombea Uwakilishi wakati wa hafla ya utowaji wa fomu hizo kwa Wagombea wa nafasi hizo.
Wagombea Uwakilishi na Udiwani wakimsikiliza Afisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akitowa maelezo ya fomu za Wagombea wakati wa hafla ya kukabidhi fomu kwa Wawania Nafasi za Uwakilishi na Udiwani Zanzibar.
Afisa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Ndg Mohammed Ali Abdallah akimkabidhi fomu ya kugombea Uwakilishi Jimbo la Chumbuni Zanzibar kupitia Chama cha ADC Bi. Mashavu Juma Ali,  
Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar kupitia Chama cha ADC Bi. Tatu Khamis Haji, akikabidhiwa Fomu ya kugombea Uwakilishi wa Jimbo hilo kutoka kwa Afisa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mjini Unguja Ndg Mohammed Ali Abdallah, hafla hiyo imefanyika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya Maisara Zanzibar. 
Afisi Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya Mjini Ndg Mohammed Ali Abdallah akimkabidhi fomu Mgombea wa Chama cha ADC Jimbo la Jangombe Zanzibar Bi. Fatma Mohammed Hassan ili kupeperusha bendera ya Chama chake.
Mgombea Udiwani Wadi ya Magomeni Jimbo la Magomeni kupitia Chama cha ADC Bi Bimkubwa Mohammed Nassor akikabidhiwa Fomu yake ya kuwania Udiwadi wa Wadi hiyo na Afisa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mjini Unguja Ndg Mohammed Ali Abdallah.kupeperusha bendera ya Chama chake kwa nafasi ya Udiwani Magomeni.