Tasaf iwe mbali na siasa

WANASIASA wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutotumia mpango wa
Tasaf awamu ya tatu kujitangaza na wautumie mpango huo kuhakikisha
jamii inabadilisha maisha na kuwa na kuondoa kaya zenye umaskini
uliopilitiza.

Wito huo umetolewa na Katibu tawala wa wilaya ya Makete, Joseph Chota,
kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, wakati akifungua warsha kwa
wawezeshaji wa mpango wa Tasaf awamu ya tatu ambao unatarajia kunusuru
kaya zilizo na umaskini ulio pitiliza katika halmashauri mbalimbali.

Chota alitoa onyo kwa wanasiasa wilayani humo kutumia mpango huo kwa
manufaa ya kujitangaza kisiasa na amewataka kutumia mpango huo
kunufaisha wananchi kwa  kuzibaini kaya zilizo na uhutaji na walengwa
wa mpango huo.

"Natoa wito kwa wanasiasa kuto tumia mpango huu kisiasa na watumie
mpango huu kuhakikisha wananchi wake wale waliopo katika kiwango cha
chini cha umaskini kubadisisha mfumo wao wa maisha," alisema Chota.

Alisema kuwa wanasiasa wanawajibu wa kusaidiana na wawezeshaji wakati
wa kutamua kaya zinazohitajika kuingia katika mpango huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Ukaguzi, Christopher Sanga Tasaf kwa niaba
ya mkurugenzi wa Tasaf,  alisema kuwa mpango huo kwa halmashauri ya
makete utaanza kwa asilimia 70% kwa utekelezaji na kumalizia asilimia
zilizo baki baada ya kumaliza awamu hiyo.

"Kwa kuwa si rahizi kufikia halmashauri yote kwa wakati mmoja hivyo
halmashauri itaanza kwa asilimia 70 na kumalizia vijiji vilivyo baki
mpango huu utafikia kila kijiji na mtaa wa halimashauli iliypo katika
mpango," alisema Sanga.

Alisema kuwa mpango huu ni nchi nzima na hakuna sehemu iliyo achwa na
kuw awakati wa kutambua maeneo ya kufanyia kazi kuna halmashauri
ambazo zilikuwa bado haziaundwa lakini zitafikiwa kupitia halmashauri
mama.

Alisema kuwa wananchi katika mpango huu wategemee kuondoka katika
mazingira magumu wanayo ishi na hasa kaya zile zilizo na umaskini
uliopitiliza, na mpango huu unawanufaisha wanakaya tofauti na uli wa
awamu ya kwanza nay a pili ambapo ulikuwa unahudumia kijiji.

Alisema: "awamu zilizo pita mpango ulikuwa unanufaisha baadhi ya watu
na kuwa kwa kuwa katika huduma za afya kuna watu wanatengwa na kuwa
kuwa sasa tutalenga kaya hivyo watu watakuwa na ruzuku ambayo
itawafanya waimalike kifaya na kielemu".

Aliongeza kuwa katika mpango huu sehemu walizo fanya majalibio
wakikumbana na changamoto ya kuzikataa fedha hizo kwa imani ya kuwa ni
za Freemason kwa madai kuwa serikali haiwezi kutoa pesa kwa wananchi
bila ya kufanya chochote na wakabaini njia ya kupambana na changamoto
hiyo kwa kuwashirikisha wananchi wakati wa kutambua kaya maskini.