WATUMIAJI wa huduma za kibenki nchini wametakiwa kuhakikisha wanalinda namba za siri katika kadi zao za benki na kutompa mtu yeyote hata kama wanaaminiana kwa kiasi gani.
Akizungumza katika semina ya wanahisa wa CRDB mkoa wa Njombe Mwezeshaji katika semina hiyo, Mgwagi Steven, alisema kuwa kumekuwa na kesi mbalimbali za kuibiwa pesa na ndugu katika mashine za kutolea pesa.
Alisema kuwa wananchi wanao tumia kadi katika utoaji wa pesa wanatakiwa kuwa makini na kadi zao na kutotoa namba ya siri kwa mtu yeyote hata kama anamuamini kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wamepokea kesi nyingi zikihusisha baba na mtoto marafiki na mtu na mkewe au mumewe kuibiwa pesa kupitia mashine za kutolea fedha.
“Tumepokea kesi nytingi za watu kuibiwa pesa na ndugu wanao waamini kwa kuwa waliwapa namba za siri za kadi zao za ATM ambapo wamekuwa wakiibiwa kati na kwenda kutolewa pesa zao,” alisema Steven.
Aliwahadhalisha wananchi kuhusiana na kutoa taarifa zao za benki kwa nyia ya simu au kujibu sms au barua pepe na kuwa benki zote sasa zinatoa huduma zao za kubadilisha taarifa kwa kufika moja kwa moja benki na sio kwa njia hizo.
Alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiibiwa kwa njia ya mtandao kwa kutoa taariufa zao kwa mtu anayejitambulisha kuwa yeye anatoka benk Fulani na kumpa taarifa zako na kasha kufanya uharifu ya kimtandao.
Alisema kuwa kwa sasa wizi wa mitandao umedhibitiwa kama mtu hata toa taarifa zake wa benki hovyo na kuwa wengi walkio kuwa wakiibiwa kwa nyia ya mtandao walikuwa wakiulizwa walikkuw awakikili kutoa taarifa kwa njia za Barua pepe ama kwa kupigiwa simu na watu wanao dai kuwa ni wafanyakazi wa benki.