LICHA ya serikali kudaiwa na waalimu pesa za madeni mbalimbali yakiwemo ya malimbikizo ya mishahara na pesa za rikizo, mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba amesema kuwa waalimu waishi kwa matumaini na kuvumilia kwani serikali inatambua kuwa inadaiwa.
Kauli hiyo aliitoa juzi katika uchaguzi wa chama cha walimu Tanzania (CWT), wilaya ya Njombe, ambapo katika uchaguzi huo pia kitengo cha wanawake walipata uongozi.
Dumba akifungua uchaguzi huo alisema kuwa walimu waishi kwa matumaini ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi wakati wanasubili serikali kuwapatia pesa wanazo idai serikali.
Alisema kuwa walimu waendelee kufanyakazi bila kusitasita kuwa ili kuhakikisha watoto wanafauru na serikali wakati inafikilia kiuwapatia madai yao wanayo idai serikali.
“Walimu hakikisheni mnafanya kazi kwa weledi na wanafunzi kuwafaurisa, napenda kusema kuwa wazazi wetu zamani walikuwa tupa matumaini kuwa tusubiri chakula wakati wamepika mawe ili watoto wasikate tama hivyo walimu hakikisheni mnafanyakazi na kuishi kwa matumaini,” alisema Dumba.
Kwa katibu wa chama hizo wilaya ya Njombe, Salama Lupenza akimkaribisha mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa walimu wamaidai pesa serikali hasa zikiwa ni pamoja na zamalimbikizo ya mihashara.
Alisema kuwa mbali na kuidai serikali mabilioni ya pesa wamekuwa wakisumbuliwa wakati wa kuchukua pesa za kwenda rikizo ambapo mara zingene wamekuwa wakizikosa pesa hizo.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti aliyechaguliwa katika uchaguzi huo na kuwa mwenyekiti wa CWT wilaya ya Njombe, Shaban Ambindwile alisema kuwa suala la kuto kuwapo kwa pesa za kwenda likizo ni kuwaonea walimu.
Alisema kuwa serikali imekuwa na pesa za zarula lakini za walimu kwaajili ya likizo hazipo na mambo mengine huwa yanafanyika.
“Kuna siku kama serikali itaendelea kuto lipa pesa kwaajili ya likizo kuna siku hatutaenda likizo ya Januari na kwenda juni tuone kama mambo yataenda,” alisema Ambindwile.
Alisema kuwa serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa walimu wanapatiwa stahiki zao wakati wote ili waendelee kujenga taifa lililoimala kwa kutoa elimu bora bili kuwa na vikwazo.