STIKA ZA MAEGESHO FEKI ZAENEA NJOMBE, ALIYE GUSHI ASHIKILIWA



Katika Hali Isiyo ya Kawaida Zoezi la Oparesheni ya Ukamataji Magari Yasiyo Kuwa na Stika za Maegesho Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Limeanza Kuingia Doa Kufuatia Kuwepo Kwa Stika Bandia Ambazo Zimeanza Kukamatwa Kwa baadhi ya Madereva.

Akizungumza na waandishi wa habari Wakala wa Zoezi la Ukusanyaji Mapato ya Stika Hizo Zabron Mbeni Amesema Kuwa Hali Hiyo Inakuja Kufuatia Kuwepo Kwa Utovu wa Nidhamu Kwa Baadhi ya Vijana Wake Ambao Walisimamishwa Kazi Kwa Kufanya Kazi Kinyume na Utaratibu.
 
Bwana Mbeni Amesema Kuwa Vijana Hao Mara Baada ya Kusimamishwa Kazi Kutokana na Utovu wa Nidhamu Waliiba Stika Hizo na Kuzidurufu Kupitia Kompyuta Kisha Kuanza Kuziuza Kwa Bei ya Chini Kwa Madereva Mbalimbali.

Amesema Tatizo Hilo Limegundulika Baada ya Kuanza Kwa Oparesheni Hiyo Iliyosababisha Kukamatwa Kwa Baadhi ya Magari Yenye Stika Bandia Zinazogharimu Kiasi Cha Zaidi ya Shilingi Milioni Moja.

Aidha Ametoa Wito Kwa Mmiliki wa Chombo Chochote Cha Usafiri Ambacho Kinastika Tofauti na Zile Ambazo Zinafahamika Kuzirejesha na Kwamba Kila Mmoja Anapaswa Kufika Katika Ofisi za Wakala Huyo Mjini Njombe Ili Kulipia Stika Ya Gari Lake Au Pikipiki.


Hata Hivyo Amewaomba Wamiliki wa Magari Hayo Kuondoa Hofu Juu ya Zoezi Hilo na Kwamba ni Vyema Kila Mmoja Akaepusha Hofu Hiyo Kwa Kufika Ofisini Kulipia Kwa Hiari na Kwamba Kijana Huyo Tayari Anashikiliwa na Jeshi la Polisi.A