Chadema waanza kampeni mjini baada ya kumaliza vijiji 42

CHAMA cha demokrasia na maendeleo Chadema kimesema kuwa kinafanyiwa hujuma baada ya mkutano wao kupitishwa Helkopta (Chopa) yenye mabango ya chama cha Mapinduzi CCM na kusababisha wananchi kuondolewa kwa umakini wa mkunao.

Akizungumza na waandishi wa habari Juzi katika Mkutano wa hadhara Mgombea wa Bubunge jimbo la Njombe Kusini Emmanuel Masonga alisema kuwa CCM inawafanyia hujuma kwa kuwa ilipanga kutaka kuvuruga mhunano wao kwa kupitisha chopa juu ya mkutano wao.

Alisema kuwa kitendo hicho kiliwaondolea umakini wananchi walio ingia katika mkutano wao na wengine kuzomea zomea mkutano huo kwa muda wa zaidi ya dakika 5 baada ya choapa hiyo kukatika mara mbili angani.

Masonga alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria, na kuwa ni hujuma za waziwazi kwa chama chake ambazo zimepangwa na CCM.

Aidha akielezea maendeleo ya kampeni za chama hicho alisema kuwa wamefanikiwa kupita vijiji 42 kati ya vijiji 44 ambavyo vyama vingine vilijua kuwa vitashinda kupitia vijiji hivyo.

“Tumefanikiwa kupita ngome nyingi za CCM, na ACT-Wazalendo katika vijiji hivyo walitegemea watashinda kupitia vijiji hivyo lakini watu walikuwa wanasema mbona hatupo mjini na mbona hatusikiki tunacho kifanya hii ni mbinu niliyo ibuni kufanya kimya kimya ili kuwahalibia CCM kuja kusituka tumeshinda,” alisema Masenga.

Alisema kuwa kupitia kampeni katika ngome za CCM walizo fanya Kimya kimya wananchi wamebadilika na kuwakubali na kueleza kuwa walikuwa hawatumii vyombo vya habari ili kuto iamsha CCM.

Alisema kuwa katika mitaa ya mjini walisubili kwa kuwa ni ngome yao hivyo wanawakubali na hawana haraka napo na wanapita kuwakumbusha tu wananchi.

Aidha Masonga alisema kuwa  wagombea wa chama chake wanakutana na vitisho kwa kipindi hiki na kuomba viongozi wa dini kuwaombea ili uchaguzi upiti salama.
Alisema akuwa wamekuwa wakiwakumbusha mara kwa mara viongozi wa dini kugusiana kuwaombea na vitisho wanavyo vipata na kuomba jeshi la polisi kuimalisha ulinzi.