IMEBAINIKA
kuwa waalimu wa sayansi katika shule za kata ni wastani wa walimu wawili na
mmoja shule nzima kitu kinacho katisha tamaa kufundisha masomo hayo na
kusababisha wengine kukata tamaa licha ya kila shule kuwa na maabara.
Akizungumza
na kituo hiki katibu wa chama cha waalimu Tanzania wilaya ya Njombe, Salama
Luprnza (Pichani) amesema kuwa kwa shule za wilaya yake zina wastani wa waalimu 2 na
mmoja anaye fundisha kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Lupenza
amesema kuwa licha ya kuwepo kwa maabara katika kila shule za wilaya hiyo
lakini waalimu ni tatizo na kuwa baadhi ya maabara hizo hazina vifaa vilivyo
kamilika na kusababisha wanafuzi wengi kukimbia masomo hayo.
Hata
hivyo Lupenza amesema kuwa anaona kuna mahari taifa lilikosea kwa kutoi toa
hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo hayo kusababisha kuwa wanafunzi wachache
ambao wanaingia wanagawanyika wengine wakienda kusomea Udaktari Uinginia na
wengine kuingia katika fani ya Ualimu.
Lupenza
anatoa wito kwa wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi ili kulikomboa taifa na
kuwa kwa sasa chama kina mpango wa kuhakikisha kuwa serikali kutoa motisha kwa
waalimu hao na kuwa hapo baadae waalimu hao huenda wakawa na mishara ya tofauti
na waalimu wengine