WALIMU wenye ulemavu
na wanawake wanakabiliwa na changamoto mbali mbali wakiwa makazini kutokana na
watu kutowaelewa vizuri na huku wengine wakifanya kwa makusudi vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Akizungumza na walimu wanawake na walimu wenye ulemavu
mbalimbali Mbunge na Mwenyekiti wa kamati ya mikopo kwa waalimu, Margret Mkanga
alisema kuwa walimu hao wanakabiliwa na changamoto hizo katika ufanyaji kazi.
Alisema kuwa walimu wenye ulemavu wajitahidi kufanya kazi kwa
makini na juhudi ya hali ya juu ili kuonyesha kuwa wanaweza kufanya kazi kuliko
hata walimu wasio na ulemavu wa aina yoyote.
Mkanga alisema yeye alipo kuwa akifundisha alikuwa akifanya
kazi kwa bidii na kuhakikisha mwanafuzi anaye mfundisha anafaulu vizuri kitu
kilicho kuwa kikimpa furaha na faraja.
Alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwazarau walimu wenzao wenye
ulemavu na kuona wao hawaweza kufundisha vizuri.
Alisema kuwa waalimu
wakubaliane na changamoto hizo kwani zina mwisho wake ambapo zitakome na
watakubalika na kila jamii.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum (CCM) Singida Dayana
Kilolo aliwataka walimu kutumia chombo chao cha CWT ili kuhakikisha wanapata
maslahi yao.
Alisema
kutokana na madai mengi wanayodai serikali,walimu wengi wamevunjika moyo wa
kufundisha watoto mashuleni kutokana na muda mwingi kushughulikia madai yao.