Zoezi la uzoaji wataka kwa kushirikiana na wananchi na mbunge viti maalumu mkoa wa njombe likiendelea
WANANCHI mkoani Njombe wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatupa taka kwa kuzitenga ili kurahisisha zoezi la uzoaji wa taka katika vizimba na taka zinazo oza kufanywa mbolea.
Akizungumza na Nipashe wakati wa siku ya wanawake mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe Lucia Mlowe ambapo ameazimisha siku hiyo kwa kuwakusanya baadhi ya wanawake wa Chadema na kupita katika madampo mbalimbali ya mji wa njombe na kuzitoa taka zake.
Mlowe alisema kuwa takataka kama zitatenganishwa zile ngunu na zile za matunda matunda zinazooza vizimba havita furika taka kwa kuwa wazoaji wa tazichukua kwa urahisi na zile zinazo oza zitatumika katika mashamba mbalimbali kama zamadi kuliko inavyo fanywa hivi sasa.
“Wananchi wajifunze kuzitenga taka zao ili taka hizi ziweze kuzolewa bila kuwapo kwa usumbufu kwa kuwa wanao ziondoa katika vizimba hawata pata shida wakati wa kuziondoa,” alisema mlowe.
Hatahivyo wanawake walio jumuika katika utoaji wa taka wameiomba halmashauri ya mji njombe kuhakikisha kuwa taka hizo zinaondolewa kwa wakati ili kuwaepusha wananchi wa mji huo ambao kipindipindu hakija ingia kisije kikaingia.
Mmoja wa wanawake hao Wema Mbanga alisema kuwu wazo hizo ni zuri kwa kipindikikifika katika mji huo kitawaathili watu wote bila kujali ni wanawake wala wanaume.
Hivyo wazo la mbunge la kushiorikian ana wanawake kuzitoa taka katika maeneo ya vizimba kwa kupunguza mrundikano huo wa taka kutawapunguzia uwezekano wa kupatikana kwa magonjwa ya mripuko.
Aidha Robari Shejamabu ni moja ya baadhi ya wanaume mkoani Njombe amesema kuwa zoezi walilolifanya wanawake hao ni la kuheshimika na kusema kuwa wanawake wakiamua wanaweza na wasisubiri kuwezeshwa.