Waandishi watakiwa kujikita kuandika habari za umma zaidi

WAANDISHI wa habari mkoa wa Njombe wametakia kujitokeza kuomba fedha za ruzuku zinazo tolewa kila mwaka na Tanzania media foundation TMF ili kuandika babari za vijijini na habari bora.

Wito huo umetolewa na afisa wa ufuatiliaji wa ruzuku wa TMF Alex Kayamba wakati wakitoa semina ya namna ya waandishi wanaweza kushiriki kupata ruzuku za uandishi wa habari za vijijini.

Alisema kuwa Ruzuku hizo hutolewa kwa mwandishi yeyote mwenye wazo zuri la habari ambalo litakuwa tofauti na kugusa jamii moja kwa moja.
“Waandishi hii ni fulsa kwenu ya kufanya habari za vijijini ambazo zitakuwa ni bora zilizo na maslahi kwa jamii husika na kufanya mabadiliko ya pale palipo kuwa na utendaji mbovu,” alisema Kanyamba.

Aliongeza kuwa ruzuku hizo zinatolewa kwa waandisho 30 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili na kufikisha waandishi 60 kwa msimu nchi nzima ambapo kutakuwa na mashindano ya kazi.

Na mwandishi atakaye fanikiwa kupata ruzuku hiyo atapokea jumla ya milioni 4 kwaajili ya kumuwezesha kukamilisha stori yake atakayo ifanya.

Hata hivyo mwaka huu mfumo wa uombaji wa ruzuku utaombwa kwa njia ya mtandao na kuwa mda utakapo fika mtu atakaye omba ruzuku ata jaza fomu kwenye mtandao wa TMF.

Akitoa maelezo juu ya kujasa fomu hizo kwenye mtandao afisa ufuatiliaji ruzuku TMF, Fortonata Mmari alisema kuwa waandishi wataambatanisha vitu vyote katika mtandao tofauti na miaka ya nyuma ambapo alikuwa anatakiwa kupeleka fomu hizo ofisi yao.

Mmoja waandishi mkongwe mkoa wa Njombe Zeno Lukoa alisema kuwa waandishi wachangamkie fulsa hizo kwa kuwa miaka ya nyuma hakukuwa na fulsa hizo na kuwa licha ya kupata ruzuku waandishi watapata fulsa ya kupata elimu.