Aliye susiwa kuzikwa na wanakijiji azikwa, kibali kilicho toliwa hawajalizishwa nacho

MAREHEMU aliyeuwawa kwa kupigwa na Polisi ambaye mwili wake ulisusiwa kuzikwa Juzi umezikwa huku ndugu wa marehemu wakiwa na manunguniko

Mwili huo wa marehemu ambaye aliyeuawa na polisi wa doria siku ya Jumanne usiku wiki hii mjini Njombe, Basil Mwalongo (24), umezikwa jana majira ya saa 7 mchana kijijini kwao Lugenge.


Hata hivyo ndugu wa marehemu wamesema hawaridhishiki na kitendo cha jeshi la polisi Mkoa wa Njombe kushindwa kutoa taarifa kamili juu ya sababu cha kifo cha ndugu yao.

Rose Mayemba amesema serikali ilipaswa kuweka wazi juu ya chanzo cha kifo cha mtu huyo na si kusema tu amekufa baada ya kutoka damu nyingi bila kueleza sababu za kuvuja kwa damu hizo.


Msemaji wa familia, Joseph Mwalongo, amesema baada ya juzi kususa kuuzika mwili wa ndugu yao baada ya kupewa kibali kisicho halali, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba aliwapa kibali ambacho kimesainiwa na daktari lakini hawaridhiki na sababu za kifo cha marehemu kilichotolewa kwamba alikufa baada ya kuvuja damu nyimngi.
  
Amesema mpaka sasa siku nne zimepita tangu tukio hilo kutokea lakini jeshi la polisi limeshindwa kuzungumza chochote juu ya tukio hilo hali inayopelekea ndugu na wananchi kwa ujumla kushindwa kuelewa nini kilichowafanya kukaa kimya.

Ndugu hao wamesikitishwa na jishi hilo kuto tolea taarifa ya tukio hilo la mauaji ambalo limesabishwa na Polisi.

Baadhi ya wananchi wamezungumza na Kituo hiki katika eneo la mazishi walilitaka jeshi la polisi kutoa tamko juu hatua lilizochukua dhidi ya aliyehusika na mauaji hayo.


Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Franco Kibona kuahidi kulitolea ufafanuzi jana tukio hilo lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa kwenye kikao na wakuu wa polisi wa wilaya Mkoani humo.

Juzi wakazi wa Kijiji cha Lugenge walisusa kuuzika mwili wa Mwalongo kwa kile kilichodaiwa kuwa serikali ilitoa kibali cha kifo kisichozingatia taratibu za kisheria hali iliyopelekea Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba kuingilia kati kufuatilia kibali hicho.

Marehemu Mwalongo aliyekuwa akiishi Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe, inadaiwa aliuawa na askari polisi wa doria kwa kupigwa risasi siku hiyo kwenye klabya ya pombe ya Nyondo mtaani hapo, na mwingine Fred Sanga kujeruhiwa.