HALI ya biashara kwa wafanyabiashara mkoani Njombe imenekana kuwa ngumu kuelekea msimu wa sikukuu kutokana na wakulima kushindwa kuuza mazao yao kwa bei nzuri na kujikita kusomesha watoto baada ya matokeo ya darasa la saba kutolewa.
Wakiuzungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara na wakulima wa mazao mbalimbali mkoani njome wamesema sikukuu ya mwaka huu hali ni mbaya mzunmguko wa pesa umekuwa hauendani na miaka ya nyuma.
Mmoja wa wafanyabiashara anayefanya biashara ya mchele katika soko kuu la mkoa wa Njombe, Maganga Mbilinyi, amesema kuwa kwa mwaka huu biashara imekuwa tofauti na miaka yote ya hapo nyuma kutokana na wanunuzi kuwa ni wachache na bei zimebaki ni zilezile za miezi mitatu iliyopita.
Amesema kuwa biashara hiyo ugumu wake unachangiwa na kuwapo kwa bei ndogo za mazao kwa wakulima kitu kinacho sababisha wateja wao ambao wengi wao ni wakulima kushindwa kufika sokoni kufanya manunuzi.
Wafanyabiashara hao ambao ni Maganga Mbilinyi na Rajay Ngole Wamesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakitegemea kuuza mazao ili kufanya manunuzi.