WANANCHI mkoani Njombe wameliomba jeshi la Polisi kuwa karibu na wananchi katika msimu huu wa sikuu kuu ambazo zimekuwa na matukio mengi ya kiharifu ili kulinda amani na kupambana na waharifu kwa kufanya dolia mbalimbali katika mitaa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa mkoani Njombe, wamelitaka jeshi la polisi kuimarisha dolia ambazo wamekuwa wakizifanya ili kudhibiti matukio ya uharifu katika mkoa huo kwa kushirikiana na wananchi na kufika kwa haraka katika matukio watakapo hitajika.
Diwani wa kata ya Njombe mjini Agley Mtambo alisema kuwa katika msiku huu wa sikukuu kuwekuwa na matukio mengi ya uharifu katika maeneo mbalimbali ya miji hapa nchini hiyo jeshi la polisi lihakikishe lina imarisha ulinzi kwa kufanya dolia.
Mtambo aliwageukia wazazi na kuwataka kuhakikisha wao pia wanakuwa walinzi katika nyumba zao hasa kwa kuto ondoka wote hasa kuelekea katika mikesha mbalimbali ambayo imekuwa ikifanyika.
Alisema kuwa pia wazazi wanawajibu wa kuhakikisha watoto wao wanapo toka kwenda kusheherekea wahakikishe wanawaachia chini ya uangalizi wa mtu mzima ili kupunguza matukio ya kupotea kwa watoto ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika sikukuu kubwa kama hizo za mwisho wa mwaka.
Kwa upande wa jeshi la polisi mkoani humo limesema kuwa litakuwa na doria za aina tatu katika mitaa tofauti ikiwa na lengo la kuimarisha ulinzi na kuhakikisha sikukuu zinatawariwa na amani.
Kamanda wa polisi mkoani Njombe Fulgence Ngonyani alisema kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha amani inakuwepo katika mishesha yoto na kuwa na ulinzi katika makanisa yote yanayo azimisha kuzaliwa kwa mwokozi wao hii leo katika sherehe za Krismasi na katika mkesha wa Mwaka mpya.
Alisema kuwa watakuw ana dolia za askali watakao kuwa kwa miguu, polisi watakao kuwa katika pikipiki na askali watakao kuwa katika magari kuzunguka mji mzima na viunga vyake usiku kucha wa jana na siku mzima ya sikukuu ya Krisimasi na usiku wa mkesha wa Mwaka mpya na siku ya mwaka mya.