Mgombea Ubunge ACT Wazalendo anusulika kupigwa na watu anaodai ni CCM










MGOMBEA wa ACT-Wazalendo jimbo la Njombe Kusini, Emilian Msigwa amenusulika kupigwa na watu wanao daiwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi akiwa katika mkunano wa kampeni za uchaguzi huku mfuasi mmoja wa chama hicho kukimbizwa Hospitalini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mgombea huyo alilalamika kuhusiana na vurugu hizo Juzi akisema kuwa zilitokea juzi katika mkutano wake uliokuwa ukifanyika katika kijiji cha Yakobi cha jimbo hilo mkoani Njombe.

Msigwa alisema kuwa katika kata ya yakobi amekuwa akipata shida ya kufanya kampeni katika vijiji vyake kutokana mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia CCM kuweka vikwazo vya kuzuia mikutano ya chama hicho kwa kuweka naye ratiba zake na kufanya hujima na watendaji wa vijiji hivyo.

Alisema kuwa mgombea wa udiwani awali wlitakiwa kufanya mkutano katika kijiji hicho alicho letewa vurugu lakini alizuia gari ya matangazo na kusema kuwa katika kijiji hicho kuna kampeni za CCM kwa mujibu wa ratiba.

Alisema kuwa baada ya kufikishana katika Ofisi za kijiji cha Yakobi alibadilishiwa ratiba na kuwa mgombea huyo alikuwa  na ratiba ya siku nzima katika kijiji hicho hivyo siku ya Juzi baada ya kupangiwa ratiba kwa siku hiyo akiwa katikati ya mkutano aliona gari ya iliyo na bendela za CCM iliingia katika mkutano wake.

Akielezea mkasa huo alisema kuwa baada ya gali hiyo kuingia katika mkutano wake ilisimama kati kati ya jukwaa lake na upande walio simama wananchi na kuwa baada ya hapo uliwashwa muziki wa CCM na baada ya muda kuna watu walio na miili mikubwa (Mabaunsa) walishuka katika gali na kumfuata mfuasi wa chama hicho ambaye ni maarufu aliye toka chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.

Alisema kuwa mfuasi hiyo Ally Mhagama maarufu Sagasaga alivamiwa na watu hao na kuanza kupigwa kasha kupelekwa katika gari ya CCM wakitaka kuondoka nae Wananchi wa liokuwepo kwenye mkutano hawakukubari waliamua kuaza kupambana nao.

Alisema wakati vurugu hizo zinatokea Polisi wa kulina uvunjifu wa amani katika mkutano wake hawakuwepo na kuwa yeye alikimbilia kweye gali akiwa anajiokoa.

Alisema kuwa wakati vurugu zinaendelea Mgombea Udiwani kata ya Yakobi alionekana eneo la tukio akiwa ameshika mawe mawaili akitaka kuwarushiwa wananchi na baada ya muda polisi walifika eneo la tukio.

Akizungumzia ulizi wa polisi katika mikutano yao alisema kuwa katika mikutano yao mingi ya vijiji huwa wanaenda bila ya kuwa na polisi kutokana na umbali wa maeneo na kuwa na imani ya kuwa na amani katika maeneo hayo na kusema kuwa mikutano ya mjini huwa wanakuwa na Polisi.


“Katika mikutano yetu yote wanayo ya vijiji huwa tunafanya bila ya kuwa na polisi kwa kuwa hawawezi kufika eneo la kampeni kutokan ana ubali wa baadhi ya maeneo na kuwapo na amani katika vijiji vingi lakini kwa maeneo ya mjini huwa tuna kuwa na askali na katika maeneo tunaona viashiria vya ukosefu wa amani huwa tuna waambia polisi wanakuwepo,” alisema Msigwa.

Msigwa aliongeza kuwa ameshiriki chaguzi nyingi lakini hajawahi kuona CCM wanafanya vurugu lakini vyama vingine lakini vyama vingine ni kawaida lakini mwaka huu ni tofauti na kuwa CCM wamebanwa.

"Chama cha mapinduzi mwaka huu kimebanwa na kinatumia mbinu mbalimbali kama zilivyonifanyia mimi mwaka huu," aliongeza Msigwa.

Akizungumza na Nipashe kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Wallboard Mtafungwa,   kwa njia ya simu alisema kuwa tukio hilo limewafikia na kuwa wanalifanyia uchunguzi huku akisema kuwa katika mkutano huo kulikuwepo na askari ambao haikuwa rahisi kufahamika.

Aliongeza kuwa jeshi hilo bado halijajua ni wakinanani wahusina kwa kuwa baada ya tukio walitokomea kusiko julikana.