MKUU wa mkoa wa NjombeDr. Rehema Nchimbe amewataka wakazi wa mkoa huo kuvuka mwaka wakiacha maovu yote, na kuingia mwaka mpya wakiwa wasafi bila kufanya maovu waliyo yafanya mwaka huu unaoisha.
Akizungumza katika tamasha la kufungamwaka lililoandaliwa na mkuu huyo wa mkoa likilenga kufanya uimbaji, alisema kuwa mkoa wa Njombe unatakiwa kuvuka mwaka bila kuwa na Falao.
Alisema kuwa mkoa huo wenye lasilimali nyingi za madini mbalimbali mwaka unaoanza fulsa hizo zifunguke kwa wananchi na wanufaike kwa mavuno ya maliasili za thamani zilizopo katika mkoa huo.
“Mkoa wa Njombe kwa mwaka ujao unatakiwa kuwa lango la uchumi la taifa kwa wananchi wake kuwa na maendeleo na kuwa na amani na kuhakikisha kuwa nawanufaika na madini yaliyopo katika mkoa huu, wananchi mvuke mwaka huu mkiwa bila kuwa na falao wa ufisadi, falao wa ubadhilifu, falao wa uvivu, mfuke mkitarajia kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo,” alisema Dr. Nchimbi.
Dr. Nchimbi alisema kuwa wananchi kwa mwaka ujao wavuke bila kuwa na maovu yaliyo fanyika mwaka jana na kuwa mkoa huu unarasilimali nyingi wananchi na viongozi mbalimbali wakishirikiana kwa pamoja watanufaika na utajili uliopo.
Aliufananisha ufisadi na utawala uliozingumziwa katika Biblia kati ya wamisri na Waizrael ambao waizraeri walivuka bahari na kuwaancha wamisri wakimezwa na bahario na kuwa kuvuka kwa waisraeli alifananisha na kuvika mwaka.
Kwa upande wake askali wa polisi jamii Inspekta, Issa Asali alisema kuwa wananchi katika msimu huu wa sikukuu hizi za kumaliza mwaka wanatakiwa kutoa ushirikiana kwa jeshihilo kwa kutoa taarifa wanapo ona kuna fununu za uharifu ambapo alisema kuwa katika sherehe hizi kumekuw ana uharifu wa hali ya juu.
Alisema kuwa jeshi la polisi litapambana usiku kucha katika mikesha yote kupamba na mafarao ambao ni majambazi wezi vibaka, na wadokozi wa usiki na kuwa watakesha kwaajili ya wananchi.
Katika tamasha hilo lililoandaliwa na mkuu wa mkoa liliwashirikisha wanakwaya kutoka katika makanisa mbalimbali ya mkoani humo na kutoa burudani ya uimbaji ambao mkuu wa mkoa wa Njombe aliwaalika wananchi mbalimbali kuburudika katika sherehe hizo zilizo fanyika ukumbu wa Turbo mjini Njombe.